Author - Leila

Ugaidi wa Kidijitali

JINAI ya ugaidi wa kidijitali, bado hatujaupa: ▪︎ Jina ▪︎ Utambulisho kuwa upo, na unaleta madhara makubwa kwa walengwa/victims ▪︎ Uainishi ▪︎ Fungu kwenye Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mitandao ya Kijamii ▪︎ mbinu za kutambua jinai hii inatokea na hatua za kuchukua iwapo tunalengwa sisi kwenye ugaidi wa kidijitali ▪︎ Kuwa wanawake watu wazima, na mabinti, ndiyo wanakuwa waathirika...

Grooming- Kurubuni Watoto

PAMETOKEA msamiati mpya kwenye harakati za kulinda watoto dhidi ya kunajisiwa. Neno Grooming- Kurubuni ndiyo linalotumika kuelezea jinsi mtu mzima anavyotumia ghilba ili kumrubuni mtoto, na kisha kumnajisi kwa mfululizo. Grooming- Kurubuni huchukua taswira kila aina, ili mtu mzima, aweze kumpata mtoto, wa kike au wa kiume; na kumfanyia vitendo vya unajisi. Mfano: ■ Kufanya urafiki na mtoto,...

BIMA

TUMEAMBIWA sisi wananchi wa Tanzania kuwa tunaletewa mfumo mpya wa malipo ya tiba; ambao utakuwa kwa mfumo wa Bima ya Afya. Tumeambiwa kuwa kila mwananchi alievuka umri wa miaka 18, itabidi achangie hiyo 'Bima ya Afya'. Hatujaambiwa iwapo wanafunzi waliopo vyuoni ambao wamevuka umri wa miaka 18, nao watalazimika kulipia Bima ya Afya'. Hatujaelezwa wananchi wa ngazi ya...

Je, Harakati za Ukombozi wa Wanawake Umetengeneza Mashoga?

BAADHI yetu tumekuwa wanaharakati tokea bado tunasoma shule, high school. Tulivutiwa na ile Dira ya: ▪︎ Haki kwa wote ▪︎ Usawa kwenye fursa za elimu; ajira; biashara; uongozi nk ▪︎ Ukakamavu kwa mabinti na wanawake, tusionewe; tusifanyiwe ngono lazimishi; tusibaguliwe ▪︎ Tupewe stadi za maisha ili tuweze kukabiliana na changamoto Sisi, wanaharakati wa Afrika, hususan Afrika Mashariki, tulikaa kwa pamoja, na...

DigitALL: Ubunifu na teknolojia kuleta Haki Jinsia

Ndiyo Kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2023. Kwenye karne hii ya kidijitali, wanawake tumepiga hatua, siyo tu kwenye ushiriki wetu kuleta maendeleo jamii; bali hata baadhi ya wanawake kushika usukani kwenye ubunifu uliotokana na maendeleo ya kidijitali. Hapo hapo, tukumbuke kuwa siyo wanawake wote kwenye Taifa letu adhimu, ambao wanapata fursa ya kutumia...

Ubadhirifu na Utumiaji Mbaya wa Madaraka

BADO WABONGO hatujapatiwa elimu jamii juu ya ubadhirifu, na/au utumiaji mbaya wa madaraka. Jamii zetu hazijapewa uelewa juu ya jinai hii, ya ubadhirifu na/au utumiaji mbaya wa madaraka. Hata pale panapotokea matendo ya ubadhirifu au/na utumiaji mbaya wa madaraka; wachache miongoni mwetu tunaouelewa kuwa pamefanyika kosa, tena takriban mara nyingi au zote, linakuwa ni kosa la jinai;...

Chujio la Socrates

MWANAFALSAFA wa Yunnani, Socrates, alikuwa ana kipimo ambacho alikipa jina chujio. Kipimo hiki, kilikuwa kimewekewa pande 3, ambazo ndiyo mizani ya hilo chujio, ili wasikizaji waweze kupata taarifa yenye uhakika. Pande ya Kwanza Je, umeweza kuhakikisha kuwa unayoyasema juu ya mtu yanaukweli? Na kama yanaukweli, ulitumia mbinu zipi kufafanua, na kujihakikishia kuwa ni ukweli? ▪︎Ulishuhudia kwa macho yako? ▪︎ Anaeongelewa kwenye...

International Women’s Day IWD March 8, 2023

Messages from Leila's Cafe YES, we have made strides in moving forward the Women's Rights Agenda. Yes, we have organized ourselves, as advocates for women's rights, into a cohesive Movement. Yes, we have more women in leadership positions in Tanzania. Yes, the rights and protection of children has become a priority. Yes, women are more vocal; more visible; more assertive. Yes,...

DONDOO

■ Kwa nini wanawake wa Afrika, hususan hapa kwetu, tulianza kudharau vipodozi na virembesha vya asili, na badala yake, tukajiingiza kwenye virembesha vilivyojaa kemikali? ■ Mabibi zetu wakitumia virembesha asili, bila ya kemikali, na hawakuwa na makunyo usoni. Wakipendeza mpaka uzeeni. Sisi, tunanunua cream zenye kemikali; za bei kubwa; ambazo baadhi yao zinaleta athari kwenye afya zetu. ■ Mfano...

Criminal Justice/Haki kwenye Jinai

TAIFA letu adhimu limeanza mchakato wa kukusanya maoni ya wadau muhimu, juu ya Haki kwenye Jinai, au Criminal Justice, kwa lugha ya Kingereza. Haki ambazo sisi wananchi tunatakiwa kuwanayo na kufaidi, ni: ▪︎ Kuweza kuchukua za kisheria dhidi ya mtu/watu, waliotutendea kosa/makosa ya jinai. ▪︎ Uwezo wa kupeleka malalamishi yetu dhidi ya makosa ya jinai tuliotendewa, kwenye chombo...

MAONI

■ Wananchi tupatiwe elimu jamii juu ya maana na utekelezaji wa Criminal Justice/Haki kwenye Jinai. Hii ifanyike kupitia vyombo vya habari, hususan redio, ambayo ni chombo cha habari shirikishi, na kinawafikia 89%-93% ya walengwa; hata waliopo kwenye vitongoji ambavyo vipo kidogo na umbali. ■ Pawepo na Daftari la waliokutwa na hatia ya jinai ya unajisi wa watoto;...

Urembo Unapogeuka Athari Kwenye Afya

Tangu dahal zamani, wanawake wamekuwa wakitumia urembo wa vipodozi kama udongo mwekundu (ochre), samli, tui la nazi, nta au gundi la miti kwenye nywele, mdaa, na Vinginevyo ili wajipendezeshe. Inasemekana kuwa Malkia Cleopatra akioga kwa maziwa ya punda ili kulainisha ngozi. Aidha, akipaka usoni samli iliyochanganywa na maua ili kuondoa makunyo ya uso. Urembo ni sehemu muhimu...

Ukatili wa kijinsia dhidi ya walemavu

DESEMBA 3 tunaadhimisha Siku ya Watu wenye Uwezo Tofauti, ambao wengi wetu huwa tunatumia msamiati wa kuwaita Walemavu. Ni Siku ambayo tunatakiwa kufanya yafuatayo: ■ kutambua uwepo wa watu wenye uwezo tofauti/walemavu, na jamii inayowazunguka. ■ kufanya tathmini ya Mipango ya Taifa ya mwaka uliopita, na kuangalia tumepiga hatua ipi kwenye kuendeleza maisha ya walemavu; mapungufu yaliyopo kwenye...

Utumiaji wa Vipengele vya Sheria

KESI za unajisi wa watoto na ubakaji zimekuwepo miaka ya nyuma kabla ya kupitishwa Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998; na hata baada ya kupitisha SOSPA 1998, matukio ya uhalifu wa kingono, yamekuwa yakitendeka. Sheria tumeletewa kwa ajili ya: ■ Kuwapa adhabu wanaotenda jinai ya kingono/sexual offences. ■ Kupunguza, na hatimaye, kutokomeza kabisa matendo ya jinai ya...

Kuambukiza VVU kwa Makusudi

MWAKA 2008, Tanzania tulipitisha Sheria ya Kudhibiti Maambukizi ya VVU. Sheria hii tuliipitisha baada ya kupitisha Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI 2001. Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI 2001 ni Sera ambayo ilileta: ■ Muongozo ■ Dira ■ Mbinu juu ya kukabili VVU/UKIMWI. Aidha, Sera hii imeainisha yafuatayo: ● Uwepo wa ugonjwa wa VVU/UKIMWI kwenye Taifa letu ● Jinsi ya kujikinga, dhidi ya maambukizi ya...

Choko Choko Mchokoe Pweza

WASWAHILI huwa tunapenda 'misemo', siyo tu wakati wa maongezi na wenzetu, bali hata kwenye: ▪︎ Kanga- huwa tunaweka usemi wa mafumbo; au wakutoa salaa; au wa kusherehekea sikukuu kama Eid; au kuomba radhi; kumshukuru Mwenyenzi Mungu; na zaidi ya yote, kurusha makombora ya majibu kwa mahasimu wetu, ambao wametutendea ubaya. Wengi hujiuliza, hasa watu wa sehemu za...

Matusi ya nguoni

WACHACHE miongoni mwa wanajamii wa JMT, wanaelewa kuwa Matusi ya Nguoni ni Kosa la Jinai Hii imeainishwa kwenye Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998, kwenye Utangulizi, pale ambapo Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998, imeweka bayana kuwa SOSPA 1998 ni Sheria inayorekebisha Sheria kadha, juu ya masuala ya jinai ya kingono, ili kulinda heshima; staha;...

Nini Kifanyike Kutokomeza Mmomonyoko wa Maadili?

Wazazi/Walezi ▪︎ Watenge muda kila wiki kuwapa nasaha njema watoto na miongozo ya maisha ndani ya misingi ya maadili. ▪︎ Wasiwape watoto smart phone. Badala yake, wawapatie watoto simu za vitochi, kwa ajili ya mawasiliano. ▪︎ Wawapangie watoto muda wa kuangalia luninga; muda wa mazoezi ya shule/homework; muda wa kufanya usafi wa nguo zao na mazingira yao; muda wa...

Mipaka kwa Watoto

TUNAPOWEKEA watoto mipaka kwenye mienendo ya maisha yao, tunakuwa tunakiuka haki zao za maamuzi? Au ni njia mojawapo ya kuwapatia watoto Muongozo juu ya: • Maadili • Heshima • Kutojiingiza kwenye mambo ya kiutuzima, wakati bado ni watoto • Ulinzi • Mfumo wa maisha utakaowajenga Wanaharakati tumegawana pande 3, tupo: ▪︎ Tunaoamini watoto wanahitaji Muongozo na Mafundisho ya Kiroho/Spiritual Guidance, ili wapate makuzi...

Wanawake Wanapogeuzwa Bidhaa

TOKEA dakhari zamani, wanawake/wasichana, wamekuwa wakifanywa aina flani ya bidhaa. Hii inajumuisha: ■ Kuozeshwa kwenye umri mdogo na wazazi, ili wazazi wapate mahari kama faida ya kumpa mwanaume mzee, binti wao mdogo kwa kisingizio cha mahari. ■ 'Kuuza' mabinti kwa dalali kutoka miji mikubwa na majiji, kufanya kazi za nyumbani, na mara nyingi, huuzwa kwenye biashara haramu ya...

SHUKRANI

NYOYO zenye shibe na nafsi zenye shukrani, zinakuwa zimekidhi matakwa ya Mwenyenzi Mungu, kuwa majaribu ni sehemu ya maisha yetu, na sisi, hatutakiwi kukata tamaa; wala kuvunjika moyo; kwa sababu, hata Mitume kwenye Misahafu Takatifu, walipewa majaribu, na ilibidi waombe kwa Mwenyenzi Mungu, awavushe kutoka hayo majaribu. Tatizo letu sisi binadamu, tumeumbwa na mapungufu, ambayo huwa...

Gaslighting-Mafumbo Yakuumiza Hisia

TUMEJENGA utamaduni wa kurushiana mafumbo yanayoumiza hisia za wenzetu. Kwa Kingereza, tabia hii inaitwa Gaslighting ambayo duniani kote, imejijenga kwenye tamaduni za binadamu, wanawake na wanaume. Hapa kwetu JMT, gaslighting tumeipita majina kadha yakiwemo: ▪︎ Rusha Roho ▪︎ Mipasho ▪︎ Kuchamba ▪︎ Kusuta ▪︎ Kuchafua staha na heshima ya mwanajamii mwenzetu, kwa kuzungusha taarifa za uongo juu yake ▪︎ Masimango Hii yote, ina nia...

MAWARIDI

MAWARIDI akiniletea kila baada ya kunipiga au kunitusi. Ni njia yake ya kuniomba radhi. Siku ya Wapendanao, Valentine's Day, pia akiniletea mawaridi, na kuniambia nipake make up, ili kuficha alama za vidole vyake usoni mwangu. Pia akiniambia nivae nguo zenye kuficha alama za kipigo. Kila baada ya kunipiga, akilia na kuniomba "Baby nisamehe, sitorudia tena....

Kebehi za maumbile- Fat Shaming

BAADHI yetu tumepitia tashtiti za kebehi juu ya miili yetu. Kuanzia jinsi tulivyoumbwa; hadi uzito wa miili. Imekuwa ndiyo utamaduni siku hizi- wanawake, na mara nyingine wanaume, kukebehi miili na maumbile ya wenzao. Wengi wetu ni wahanga wa kebehi hii. Waweza kutana na mtu, wala hamfahamiani vizuri, ataanza kukuchambua kuanzia kichwa, hadi nyayo za miguu, kwa kauli yenye maneno...

Ukatili wa kijinsia kupitia mitandao ya kijamii

TOKEA ulimwengu ulipoingia kwenye karne ya kidijitali, pameanza aina kadha za jinai zikiwemo: ■ Ukatili wa udhalilishaji kupitia mitandao ya kijamii au Kimombo, wanaita Trolling Hii hutumika kwa njia ya- ▪︎ kumtusi mtu au kundi la watu, kuptitia mitandao ya kijamii, mfano Twitter; Instagram; Facebook; Club House; nk. ▪︎ kutoa taarifa za uongo; zenye kuvunja staha; heshima; hadhi; utu;...

Ukatili wa Kijinsia kwa njia ya matusi

WENGI wetu hatujaweza kuchanganua na kuweka matusi dhidi ya mwenza/intimate partner, kuwa ni njia mojawapo ya ukatili wa kijinsia ■ Tumelelewa na kufundwa kuwa Kudhalilishwa kwa kitumia maneno ya kashfa; matusi; yanayoumiza hisia, ni jambo la kawaida. Tumefundwa kustahmili, hata kama tunaumia hisia. ■ Jamii zetu zimempa mwanaume rukhsa kumtukana mwenza/intimate partner; kumbeza; kumkebehi; kumfanya ajihisi dhalili, bila...

Waleteni Watoto Kwangu

Yesu/Eissa WATOTO wanazongwa kutoka kila upande, hapa JMT kwetu. Watoto hawapo salama. Matendo ya ukatili dhidi ya watoto yanazidi kuongozeka, orodha ni ndefu: ■ Unajisi wa watoto umeongezeka kwa 80%. Kuanzia ubakaji wa mabinti; hadi ulawiti wa watoto wa kiume. Kila kukicha, tunapata taarifa ya matukio mapya ya ulawiti wa watoto wa kiume, na wa kike. Wanaofanya hivyo, ni watu wanaoaminiwa na...

Dondoo Muhimu kusaidia wenye hisia za kujiua

KWANZA kabisa, tuweke bayana yafuatayo: ■ Hapa kwetu JMT, suala la mtu kupitia hisia za kujiua, kwa kuamua kuchukua maisha yake, huwa hatulizungumzii. Na tunapolijata, ni pale mtu ameshajiua; na mara zote, huwa tunamsema kwa ubaya, huyo mtu aliechukua maisha yake. Hatuna hisia za huruma kwa mtu anaeamua kujiua. Inawezekana kutokana na mafundisho ya Imani, kuwa ni dhambi kubwa,...

BODA BODA

HIKI CHOMBO chenye jina lenye maneno mawili, kimetukomboa kwenye suala la usafiri. Siku hizi, wengi wetu hutumia chombo cha boda boda kama usafiri, na chombo hiki kimeturahisishia maisha, hususan, kwenye usafiri wetu, na wa mizigo yetu. Hii ni kwenye majiji, hadi vijijini, boda boda imekuwa 'mkombozi'. Miaka ya nyuma kabla ujio wa boda boda, wengi wetu tukipanda dala...

Ukatili dhidi ya Watoto

PAMEZUKA wimbi la ukatili dhidi ya watoto JMT Bara, na Visiwani. Matukio yanatolewa ripoti kila kukicha, kuanzia: ▪︎ Unajisi wa watoto kingono ▪︎ Vipigo ▪︎ Vitisho ▪︎ Ngono lazimishi kwa mabinti wadogo ▪︎ Ulawiti wa watoto wa kiume ▪︎ Mateso ya kihisia kwa matusi ▪︎ Mateso kutoka kwa wazazi ambao huwapiga watoto bila kiasi, au huwaacha bila ya matunzo...

UKEKETAJI wa Mabinti/Wanawake

MWAKA 1998, Tanzania ilipitisha sheria kuharamisha masuala mengi ya jinai dhidi ya wanawake, moja wapo likiwa kuharamisha ukeketaji. Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998 kwa mara ya kwanza, ilitambua: ▪︎ Uwepo wa ukeketaji ▪︎ Madhara yatokanayo na ukeketaji ▪︎ Ujinai unaotokana na ukeketaji Tanzania ni miongoni mwa mataifa ya kwanza duniani, na ni Taifa la kwanza kuharamisha ukeketaji kwa...

Kupoteza mpendwa- mtoto; ndugu; mme/mke; rafiki kwa kujiua

MARA zote, tunapopata msiba wa aina hiyo, wa mpendwa wetu kuamua kujiua, huwa tunakuwa na maswali mengi- ▪︎ Alikuwa anafikiria nini, hadi kuamua kujiua ▪︎ Kama alikuwa na tatizo, kwa nini hakusema, ili apatiwe msaada ▪︎ Fikira zipi, na hisia zipi, zilikuwa zikipita kwenye kichwa chake na nafsi yake, hadi kuamua kujiua Aidha, sisi, tunajawa na- • Simazi • Majonzi • Hisia...

Phubbing au kupuuza mtu kwa kutumia simu

PHUBBING au phone snubbing, ni msamiati mpya wa lugha ya Kimombo, unaomaanisha kumpuuza mtu kwa kutumia simu Mara ngapi tumekuwa na wenzetu maofisini, au nyumbani, au hata tukiwa ndani ya gari, tunapoongea na mwenzetu/wenzetu, anakuwa bize kwenye simu, hata hakusikisizi, wala hakuangalii? Binafsi, imeshanitokea sana, mpaka mara nyingine kupata hisia za fadhaa, ya Kudhalilishwa; kudharauliwa; kutojaliwa. Hii imetokea...

Biashara haramu ya uuzaji wa binadamu

UUZAJI wa binadamu kwenye: Utumwa Biashara haramu ya ngono Kuwatumikisha binadamu kwenye- Mashamba Migodi Majumbani Madangulo ▪︎Kuvuna viungo vya binadamu kwa ajili ya vitendo vya ushirikina, mfano, albino; watoto wachanga; watu waliozaliwa na alama flani kwenye miili yao, kama herufi M inayoonekana kwenye viganja vya mkono; nk. ▪︎ Kuwafanyisha utumwa wanaoita dondocha au misukule, kwa kuwaiba watu, na kuwapa mitishamba...

MJANE

NENO MJANE likitajwa kwenye jamii zetu, taswira inayotujia ni ya mwanamke ambaye amefupisha maisha ya mumewe. Mwanamke balanzi. Mwanamke nuksi. Kwa nini asife yeye? Hivi, ndivyo jamii zetu zilipojikita- kuwa mjane anakuwa hana thamani tena; na inawezekana yeye, ndiye aliemuua mume. Tunasahau kuwa yeye, ni miongoni mwa waathirika wakuu, pale mume anapofariki, waathirika wakiwemo na watoto; na wazazi wa huyo...

JIPE RUKHSA

TUMEZOEA kupata hisia za fadhaa na za kujilaumu, tunapotenga muda, wa kujihudumia wenyewe au kufanya mapumziko japo ya nusu saa, ili kupumua, wakati tunaendelea na shughuli zetu za maisha. Makuzi tuliopewa wanawake tokea utotoni, ni ya 'utumishi' kwa familia; jamaa; hata marafiki. Tunaambiwa utotoni kwenye familia zetu kuwa "Mwanamke bora, ni yule anaejisahau yeye mwenyewe kabisa, na...

Watoto kwenye Omba Omba

MWAKA jana 2021, tulipata taarifa kuwa wapo watoto kutoka JMT, waliopelekwa Kenya, kufanya kazi ya omba omba. Aidha, tulipata taarifa kuwa watoto hao ni miongoni mwa wale wanaosafirishwa kwenye biashara haramu ya uuzaji wa binadamu. Binafsi, nilihojiwa na redio ya VOA kuhusu suala hili, na mwanahabari mwenzangu wa Kenya; na mwanaharakati wa ulinzi wa watoto huko Kenya;...

SHUKRANI

NYOYO zenye shibe na nafsi zenye shukrani, zinakuwa zimekidhi matakwa ya Mwenyenzi Mungu, kuwa majaribu ni sehemu ya maisha yetu, na sisi, hatutakiwi kukata tamaa; wala kuvunjika moyo; kwa sababu, hata Mitume kwenye Misahafu Takatifu, walipewa majaribu, na ilibidi waombe kwa Mwenyenzi Mungu, awavushe kutoka hayo majaribu. Tatizo letu sisi binadamu, tumeumbwa na mapungufu, ambayo huwa...

PANAHITAJIKA

■ Sera ya Taifa ya Ustawi wa watu wenye ulemavu wa aina zote, kuanzia ulemavu wa viungo hadi ulemavu wa ngozi na kusikia ■ Panatakiwa iundwe Baraza kwa ajili ya mustakabala wa watu wenye ulemavu. Baraza lijumuishe- • Viongozi wa watu wenye ulemavu • Viongozi wa Imani • Wanaharakati wa Haki Jamii • GoT ■ Panatakiwa pawepo na Dawati...

TUJIULIZE

Je sisi wanawake ni malaika? Au tunachangia kwa kiasi fulani, kwenye mmonyoko wa mahusiano ya kindoa/kimapenzi? TULIPOANZA harakati za kumkomboa mwanamke kutoka kwenye: Ndoa yenye ukatili Mahusiano ya kimapenzi yenye kuumiza nafsi, na hisia Ufinyu wa fikra, kwa kuamini kuwa 'wanawake tumeumbiwa mateso' hivyo, tukubaliane na hali tunamojikuta Kutofikiria nje ya kishubaka, kwa kuamini kuwa 'bila...

Wanawake Kupeana Sapoti

UMOJA ni nguvu, ni usemi wa Kiswahili, na ilikua Kauli Mbiu ya Taifa letu baada ya Uhuru. Umoja ni nguvu kama Kauli Mbiu iliweza kujenga Taifa madhubuti kabla na baada ya Uhuru wa Tanzania. Aidha, maudhui hayo yamejenga jamii zetu wakati wa makarne ya nyuma, kwa kuweka mfumo wa kusaidiana miongoni mwa wanajamii, wakati wa msiba; kuumwa;...

KANSA YA TITI

IFIKAPO Oktoba kila mwaka, wanaharakati wa Haki Afya huwa tunaadhimisha mwezi wa kusambaza elimu jamii juu ya saratani ya titi. Aidha, tunakumbuka wapendwa wetu; wanawake wenzetu; mabinti zetu; waliotangulia mbele ya haki, kutokana na saratani ya titi. Mwezi Oktoba inakuwa kama ni kilele cha mchakato ulimwenguni, wa kueneza elimu jamii, na uelewa juu ya saratani ya titi. Ukweli...

Self Love in Women

WE have been trained; raised; and made to believe; that when we, as women, practice self love, it is selfishness; egotism; and lack of empathy in our part. Women are always expected to be self deprecating; self denigrating; and moreover, to be giving and giving, of ourselves, until we lose ourselves. We lose our self worth. We lose...

Cyber Stalkers- Wakozi kwenye Mitandao ya Kijamii

PAMEANZA jinai mpya inayoambatana na ukuaji wa mitandao ya kijamii, inayotambulika kama Cyber Stalking kwa lugha ya Kingereza; au Ukozi wa Mitandao ya Kijamii. Bado hapa JMT kwetu, hatujaweka sheria inayoainisha jinai hii, ya Ukozi wa Mitandao ya Kijamii, japokuwa jinai hii ipo, na inaweza kuhatarisha maisha ya wanajamii, hasa huyo mlengwa/target, wa ukozi. Neno ukozi limetokana...

International Women’s Day IWD March 8, 2022

Messages from Leila's Cafe YES, we have made strides in moving forward the Women's Rights Agenda. Yes, we have organized ourselves, as advocates for women's rights, into a cohesive Movement. Yes, we have more women in leadership positions in Tanzania. Yes, the rights and protection of children has become a priority. Yes, women are more vocal; more visible; more assertive. Yes,...

Sexual Harassment

IS sexual harassment an economic crime? Yes, sexual harassment is, an economic crime, in the context of: ▪︎ The impact of sexual harassment in the income of the victims/survivor ▪︎ The impact on the health of the victim/survivor, to the detriment of their earning capacity ▪︎ The loss of trained and skilled workforce to the nation ▪︎ The invasion of...

Ugonjwa wa akili

Ni suala ambalo huwa hatulizungumzii kwenye jamii zetu. Huwa tunahisi ni jambo la aibu iwapo sisi wenyewe, au mwanandugu anatatizo la ugonjwa wa akili. Ugonjwa wa akili upo wa aina kadha: 1. Schizophrenia, ugonjwa huu ni pale mgonjwa husikia sauti kichwani mwake, na huwa anasema na hizo sauti, huku jamii ikimwona anasema peke yake. 2. Anxiety Disorder, ugonjwa wa...

Depression/Hisia ya huzuni

MARA nyingi, tunapopata changamoto au mitihani ya maisha, huwa inaambatana na hisia ya huzuni; unyonge; kupoteza furaha; na kujihisi ovyo ovyo. Hisia hii ni aina ya hali ambayo inaitwa depression, na iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa na muathirika, na watu wa karibu yake, inaweza kujijenga kwenye akili; hisia; na mwili wa muathirika, hadi kuwa ni ugonjwa. Depression inaweza...

Mwanamke Jithamini. Jiamini. Jipende

TUKIFATA mrengo wa J 3 kwenye maisha yetu sisi wanawake, • J- Jithamini • J- Jiamini • J- Jipende tutakuwa tumepiga hatua kwenye maisha yetu, na kuweza kukabili changamoto za kujihisi sisi ni duni thamani- lacking in worth. Ni ukweli usipingika kuwa tunavyojichukulia sisi wenyewe; tunavyojiweka kwenye kishubaka ndani ya jamii zetu; tunavyokubali kutungiwa lebo duni; ndivyo jamii inavyotuchukulia, na...

Notes on conversations with Bibi Titi Mohamed

Bibi Titi Mohamed was a multi faceted woman, strongly rooted in the Swahili culture and traditions. A number of writers; reporters; and wannabe have tried to write on Bibi Titi Mohamed, but all of them have ensconced her in the visage of the politician, the activist for Uhuru, the woman who allegedly committed treason. In the conversations...