DigitALL: Ubunifu na teknolojia kuleta Haki Jinsia

DigitALL: Ubunifu na teknolojia kuleta Haki Jinsia

Ndiyo Kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2023.

Kwenye karne hii ya kidijitali, wanawake tumepiga hatua, siyo tu kwenye ushiriki wetu kuleta maendeleo jamii; bali hata baadhi ya wanawake kushika usukani kwenye ubunifu uliotokana na maendeleo ya kidijitali.

Hapo hapo, tukumbuke kuwa siyo wanawake wote kwenye Taifa letu adhimu, ambao wanapata fursa ya kutumia nyenzo na ujuzi wa kidijitali, ili kujiendeleza; na pia kuweza kushiriki kikamilifu kwenye:

▪︎ Stadi za utumiaji nyenzo za kidijitali.

▪︎ Nyenzo kama kompyuta; simu za viganja; ili kuweza kujenga uwezo wao kwenye matumizi ya kidijitali na kurahisisha maisha yao na jamii zao, kwenye ngazi ya jamii.

▪︎ Wanawake kufanyiwa uharamia wa ukatili wa kijinsia kupitia nyenzo ya kidijitali, mama kubandikiwa kashfa za uzushi, kupitia mitandao ya kijamii; wakati tunaambiwa kuwa maendeleo ya kidijitali ndiyo mkombozi kwa wanawake; lakini sasa, imegeuka silaha ya kuchafua hadhi; staha; heshima; utu; wa wanawake.

Wanawake tunahitaji:

▪︎ Ulinzi kupitia vyombo vya kusimamia sheria, ili tusitukanwe kwa kutumia nyenzo ya kidijitali.

▪︎ Stadi, ili tuweze kutumia fursa ya kidijitali, na kuleta maendeleo yetu na ya jamii zetu.

▪︎ Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Kijamii 2015, iandikwe kwa lugha nyepesi; kwa Kiswahili; na pawekwe michoro, iwe njia ya elimu jamii juu ya Sheria zetu, hususan, Sheria ya Jinai ya Mitandao ya Kijamii.

Hatua stahiki za kisheria, zichukuliwe dhidi ya watu wanaotumia majukwaa ya mitandao ya kijamii, ili kudhalilisha wenzao.

Together, we can make it happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *