Biashara haramu ya uuzaji wa binadamu

Biashara haramu ya uuzaji wa binadamu

UUZAJI wa binadamu kwenye:

Utumwa
Biashara haramu ya ngono
Kuwatumikisha binadamu kwenye-

  • Mashamba
  • Migodi
  • Majumbani
  • Madangulo

▪︎Kuvuna viungo vya binadamu kwa ajili ya vitendo vya ushirikina, mfano, albino; watoto wachanga; watu waliozaliwa na alama flani kwenye miili yao, kama herufi M inayoonekana kwenye viganja vya mkono; nk.

▪︎ Kuwafanyisha utumwa wanaoita dondocha au misukule, kwa kuwaiba watu, na kuwapa mitishamba aina ya mihadarati, ili wasahau makwao; na pia kuwapa ulemavu wa kauli, wasiweze kuongea.

▪︎ Kuwafanyisha kazi za nyumbani bila malipo, hapa JMT; au kuwasafirisha kwenda mataifa ya nje, ambapo wanatumikishwa kama watumwa; bila ya ujira; mapumziko; mawasiliano na familia zao.

▪︎ Kuuza binadamu kwenye udalali wa kuwatafutia ajira, na huyo ‘mnunuzi’ alietafutiwa mfanyakazi hulipa ‘komisheni’ kwa dalali.
Aidha, dalali huchukua 25% ya ujira wa huyo ‘alieuzwa/alietafutiwa ajira’.

 

▪︎ Kuvuna viungo vya binadamu kama-
> figo
> moyo
> macho
ili wauziwe matajiri, ambao wanahitaji kupandikizwa viungo aina hiyo.

▪︎ Kuwatumikisha watoto kwenye ‘biashara’ ya omba omba.
Mara nyingine, huwapa ulemavu hao watoto, ili watoa sadaka wawahurumie.

Uuzaji wa binadamu umeundiwa Sheria hapa kwetu, The Anti Persons Trafficking Act 2008, kwa sababu vitendo vya uuzaji wa binadamu vimeongezeka.
Mara nyingine, sisi, wananchi wa kawaida, tunashiriki kwenye biashara ya uuzaji wa binadamu, bila ya kujitambua.
Mfano, tunapopeleka nauli vijijini ili tuletewe wafanyakazi wa nyumbani, sisi tunachukulia kuwa ‘tunaajiri’ mfanyakazi wa nyumbani, hatufahamu huyo binti amepatikana vipi, kutoka kwao, hadi kufika kwenye majiji, na kufika majumbani mwetu, ambapo tunawaajiri kama wafanyakazi wa nyumbani.

Mduru wa uuzaji binadamu ni mpana, na mara nyingi, huunganisha mataifa kadha kwenye mzunguko wa kuuza binadamu wenzetu.
Huwa haituingii kwenye akili au hisia kuwa- tulioletewa kuwa wafanyakazi wa nyumbani, wamenunuliwa kutoka familia zao, kwa mikataba feki kuwa huyo binti anachukuliwa mjini kufanya kazi, na pia kusomeshwa.
Mara zote, haiwi hivyo!
Tena afadhali kwa wanaoajiriwa majumbani kwa familia za Kitanzania.
Wale wanaosafirishwa kwenda mataifa ya nje, ndiyo wanapata uonevu mkubwa, kwenye utumwa mamboleo.

Tujadili

Together We Can Make it Happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *