Phubbing au kupuuza mtu kwa kutumia simu

Phubbing au kupuuza mtu kwa kutumia simu

PHUBBING au phone snubbing, ni msamiati mpya wa lugha ya Kimombo, unaomaanisha kumpuuza mtu kwa kutumia simu

Mara ngapi tumekuwa na wenzetu maofisini, au nyumbani, au hata tukiwa ndani ya gari, tunapoongea na mwenzetu/wenzetu, anakuwa bize kwenye simu, hata hakusikisizi, wala hakuangalii?
Binafsi, imeshanitokea sana, mpaka mara nyingine kupata hisia za fadhaa, ya Kudhalilishwa; kudharauliwa; kutojaliwa.
Hii imetokea kutoka kwa wanandugu; rafiki; mara nyingine, hata kutoka kwa watoto ambao ni wadogo, wengine miaka 12.
Wanakukaushia ukavu makopa, wanapoangalia simu zao; mara wacheke, mara waseme na simu, mara watoe milio ya kusikitika, mara miguno.
Wakati huo unapokuwa umechuniwa, wewe, unabaki kuwa mshiriki wa sogozi la upande mmoja- wa kwako.
Kila unavyojaribu kusema na mwenzako/wenzako, wanakuwa hawakusikii, wapo bize kwenye simu zao, kupitia mchakato wa phubbing.
Unaweza kaa kungoja jamaa apate wasaa wa kuongea na wewe, lakini hata yafike masaa 3, bado unakuwa phone snubbed.
Jamaa yupo kwenye mode ya phubbing, hakusikii, wala hakujali.
Imefikia sasa hata wazazi na watoto wanafanyiana phubbing.
Wanandoa wanafanyiana phubbing.
Hata kwenye nyumba za ibada na vilioni, hii phubbing imekuwa jambo la kawaida.

Phubbing ilianza kama dharau, sasa inageuka kuwa ugonjwa, tena ugonjwa wa akili, ambao madhara yake tumeanza kuyaona kwa kuvunjika kwa mfumo wa kuheshimu wenzetu tunapokuwa nao.
Aidha, kuvunjika kwa mfumo wa familia na wa jamii.
Hatusikizani.
Kila mmoja wetu yupo kwenye simu.
Tumepandwa na mzuka wa simu.
Mara nyingine mume na mke wanaweza kuwa sebuleni kwako, afu, wanarushiana meseji, unajihisi kana kwamba wanakusengenya wewe!
Inawezekana.

Ulaya wameanzisha tiba ya kusaidia wanajamii wapone ugonjwa wa phubbing.
Sisi, ipo siku, tutaanza semina elekezi kutibu phubbing miongoni mwa wanajamii.
Ni ugonjwa unaotapakaa kwa kasi, tena rahisi kuambukiza.

Together We Can Make it Happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *