Ngono lazimishi inapokithiri hadi kuumiza mwanamke

Ngono lazimishi inapokithiri hadi kuumiza mwanamke

TOKEA dakhari zamani, mwanamke anachukuliwa kuwa ni-

  • Kiumbe Dhalili
  • Hana Haki Ya Melki Juu Ya Mwili Wake
  • Hana Haki Ya Kusema Kwa Mwanaume Anaelazimisha Ngono “Hapana. Sitaki Mahusiano ya Kimwili Na Wewe”
  • Sijakupenda, Na Sitakupenda, Hivyo, Kaa Mbali Na Mimi
  • Sitaki Kushikwa Shikwa Mwili Wangu Bila Ridhaa Yangu
  • Acha Kunifanyia Shambulio La Aibu, Maamuzi Juu Ya Mwili Wangu, Ni Ya Kwangu Mimi
  • Usinisogelee Karibu, Ukaweka Uso Wako Karibu Na Uso Wangu, Au Sehemu Ya Matiti Au Makalio Yangu
  • Unaponitaka Kimwili, Siyo Lazima Nikubali
  • Cheo Chako Juu Yangu Kwenye Sehemu Ya Ajira Au Sehemu Ya Elimu, Hakikupi Rukhsa, Wala Haki, Wala Ridhaa Yangu, Kwako Wewe Kulazimisha Ngono
  • Kwa Sababu Tupo Kwenye Safari Ya Kikazi Na Tumefikia Hoteli Moja, Siyo Sababu Ya Wewe Kutegemea Nitakupa Takrima Ya Ngono
  • Usichukulie Tabasamu Yangu Na Heshima Ninayokupa Kuwa Ni Ridhaa Ya Kukubali Ngono Pamoja Nawe
  • Acha Kunichafulia Jina Kwenye Jamii, Kwa Kunitangaza Mie Ni Muumini Na Mtendaji Wa Ngono Ya Jinsia Moja, Eti Kwa Sababu Nimekukataa Wewe
  • Ninapoamua Kumpa Mwanaume Penzi Langu, Na Rukhsa Juu Ya Mwili Wangu, Ni Matakwa Yangu; Utashi Wangu; Furaha Yangu; Maamuzi Yangu
  • Hapana, Sikukatai Kwa Sababu Ya Ulemavu Wa Viungo Vyako, Imetokea Sikutaki, Sikutamani
  • Ninapikukataa Kwenye Ngono Lazimishi, Siyo Kwa Sababu Unayo Kasoro Kwenye Urijali Wako, Basi Tu, Sikutaki, Na Sintoilazimisha Nafsi Ikukubali, Eti Usiumie Hisia
  • Ninapimchagua Mwanaume Wa Kumpa Ridhaa Juu Ya Mwili Wangu, Ni Hivyo, Ridhaa, Na Matamanio Yangu
  • Ukinichafulia Jina, Haimaanishi Unayotunga Juu Yangu Ni Kweli, Ni Maamuzi Yako Ya Kifedhuli, Kama Mkosaji
  • Unaponifanyia Shambulio La Aibu/Sexual Assault, Kwa Vitisho; Matumizi Ya Mabavu Na/Silaha; Ile Mshutikizie Shambulio La Aibu Bila Ya Kutegemea,  Itakupa Starehe Ya Kufikiri Umenikomoa, Lakini Starehe Hiyo Haina Raha Haswa, Wala Haina Ushindi
  • Ngono Lazimishi Inabaki Kuwa Hiyo- Ngono Lazimishi, Na Starehe Ya Kumwaga Shahawa, Haikuongezei Ujanadume, Inakupunguzia Urijali Tu
  • Unapokaa Na Wanaume Wenzio Kuwa Umenionja, Kumbe Ni Matamanio Kwenye Akili Yako Iliyojaa Hisia Za Hasira Kwa Kukataliwa, Hakukufanyi Uwe Mshindi

Leila Sheikh

November 30, 2021

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *