Ngono lazimishi inapokithiri hadi kuumiza mwanamke
TOKEA dakhari zamani, mwanamke anachukuliwa kuwa ni-
- Kiumbe Dhalili
- Hana Haki Ya Melki Juu Ya Mwili Wake
- Hana Haki Ya Kusema Kwa Mwanaume Anaelazimisha Ngono “Hapana. Sitaki Mahusiano ya Kimwili Na Wewe”
- Sijakupenda, Na Sitakupenda, Hivyo, Kaa Mbali Na Mimi
- Sitaki Kushikwa Shikwa Mwili Wangu Bila Ridhaa Yangu
- Acha Kunifanyia Shambulio La Aibu, Maamuzi Juu Ya Mwili Wangu, Ni Ya Kwangu Mimi
- Usinisogelee Karibu, Ukaweka Uso Wako Karibu Na Uso Wangu, Au Sehemu Ya Matiti Au Makalio Yangu
- Unaponitaka Kimwili, Siyo Lazima Nikubali
- Cheo Chako Juu Yangu Kwenye Sehemu Ya Ajira Au Sehemu Ya Elimu, Hakikupi Rukhsa, Wala Haki, Wala Ridhaa Yangu, Kwako Wewe Kulazimisha Ngono
- Kwa Sababu Tupo Kwenye Safari Ya Kikazi Na Tumefikia Hoteli Moja, Siyo Sababu Ya Wewe Kutegemea Nitakupa Takrima Ya Ngono
- Usichukulie Tabasamu Yangu Na Heshima Ninayokupa Kuwa Ni Ridhaa Ya Kukubali Ngono Pamoja Nawe
- Acha Kunichafulia Jina Kwenye Jamii, Kwa Kunitangaza Mie Ni Muumini Na Mtendaji Wa Ngono Ya Jinsia Moja, Eti Kwa Sababu Nimekukataa Wewe
- Ninapoamua Kumpa Mwanaume Penzi Langu, Na Rukhsa Juu Ya Mwili Wangu, Ni Matakwa Yangu; Utashi Wangu; Furaha Yangu; Maamuzi Yangu
- Hapana, Sikukatai Kwa Sababu Ya Ulemavu Wa Viungo Vyako, Imetokea Sikutaki, Sikutamani
- Ninapikukataa Kwenye Ngono Lazimishi, Siyo Kwa Sababu Unayo Kasoro Kwenye Urijali Wako, Basi Tu, Sikutaki, Na Sintoilazimisha Nafsi Ikukubali, Eti Usiumie Hisia
- Ninapimchagua Mwanaume Wa Kumpa Ridhaa Juu Ya Mwili Wangu, Ni Hivyo, Ridhaa, Na Matamanio Yangu
- Ukinichafulia Jina, Haimaanishi Unayotunga Juu Yangu Ni Kweli, Ni Maamuzi Yako Ya Kifedhuli, Kama Mkosaji
- Unaponifanyia Shambulio La Aibu/Sexual Assault, Kwa Vitisho; Matumizi Ya Mabavu Na/Silaha; Ile Mshutikizie Shambulio La Aibu Bila Ya Kutegemea, Itakupa Starehe Ya Kufikiri Umenikomoa, Lakini Starehe Hiyo Haina Raha Haswa, Wala Haina Ushindi
- Ngono Lazimishi Inabaki Kuwa Hiyo- Ngono Lazimishi, Na Starehe Ya Kumwaga Shahawa, Haikuongezei Ujanadume, Inakupunguzia Urijali Tu
- Unapokaa Na Wanaume Wenzio Kuwa Umenionja, Kumbe Ni Matamanio Kwenye Akili Yako Iliyojaa Hisia Za Hasira Kwa Kukataliwa, Hakukufanyi Uwe Mshindi
Leila Sheikh
November 30, 2021
Leave a Reply