MJANE
NENO MJANE likitajwa kwenye jamii zetu, taswira inayotujia ni ya mwanamke ambaye amefupisha maisha ya mumewe. Mwanamke balanzi. Mwanamke nuksi. Kwa nini asife yeye? Hivi, ndivyo jamii zetu zilipojikita- kuwa mjane anakuwa hana thamani tena; na inawezekana yeye, ndiye aliemuua mume. Tunasahau kuwa yeye, ni miongoni mwa waathirika wakuu, pale mume anapofariki, waathirika wakiwemo na watoto; na wazazi wa huyo...