Kupoteza mpendwa- mtoto; ndugu; mme/mke; rafiki kwa kujiua

Kupoteza mpendwa- mtoto; ndugu; mme/mke; rafiki kwa kujiua

MARA zote, tunapopata msiba wa aina hiyo, wa mpendwa wetu kuamua kujiua, huwa tunakuwa na maswali mengi-

▪︎ Alikuwa anafikiria nini, hadi kuamua kujiua

▪︎ Kama alikuwa na tatizo, kwa nini hakusema, ili apatiwe msaada

▪︎ Fikira zipi, na hisia zipi, zilikuwa zikipita kwenye kichwa chake na nafsi yake, hadi kuamua kujiua

Aidha, sisi, tunajawa na-

• Simazi
• Majonzi
• Hisia za kujilaumu, kuwa kwa nini hatukuweza kutambua mpendwa wetu anapitia kipindi kigumu
• Kwa nini hakusema, ili apate msaada

Tunapopoteza mpendwa wetu kwenye umauti, iwe kwa ugonjwa; au ajali; huwa tunajilaumu kwa kiasi fulani, na kufikiri kuwa tungeweza kuzuia umauti huo.
Inakuwa maumivu zaidi iwapo mpendwa wetu amepata umauti kwa kujiua.

Yapo mataifa kama Bara Hindi na Japan ambapo mtu kujiua imekuwa sehemu ya maisha yao.
Mataifa ya Ulaya na Marekani, wameweka mfumo wa kusaidia wenye kupitia msongo wa mawazo, hadi kuamua kujiua.
Hapa kwetu, bado hatujaweka mfumo aina hiyo, siyo tu kupitia vyombo vya serikali; au asasi za kiraia/AZAKI; lakini hata kwenye asasi za dini; hatunao mfumo wa kusaidia watu ambao wanamawazo ya kujiua.
Na iwapo mpendwa wetu anaamua kujiua, tunaichukulia kama balanzi kubwa kwenye familia.
Ndiyo maana karne za nyuma, iwapo mwanafamilia amejiua, baada ya kumpumzisha, panafanyika tambiko, ili kuleta amani na afueni kwa waliopoteza mpendwa wao kwa kujiua.
Hisia kubwa mno, ni ya lawama.
Tunalaumiana, na tunajilaumu wenyewe.
Lakini, huwa hatuongelei uamuzi wa mpendwa wetu kujiua.

Wakati umefika, wa kutafakari; kuweka mifumo ya kusaidia wanaopitia msongamano wa mawazo na ambao wanataka kujiua.

Tukumbuke, mara nyingine, jamii huchangia kupelekea mtu kuamua kujiua.
Juzi, huko Marekani, alijiua mwanamke wa umri wa miaka 30, aliekuwa super star, na mzuri, kwa sababu jamii ilikuwa inashinikiza mafanikio zaidi na zaidi na zaidi.
Hapa kwetu, juzi, Tanzania’s Sweetheart, Wema Sepetu, alichanwachanwa na mwanaume, Aristote, kuwa Wema ‘amekwisha kimaisha’.
Tena Aristote aliyasema hayo kupitia chombo cha habari, YouTube.
Wema, Mwenyenzi Mungu alimpa ujasiri, wa kubandika malalamishi kupitia akaunti yake ya Instagram.
Ilimsaidia Wema Sepetu kutoa nyongo, na kupata sapoti.
Mungu apishe mbali, angekuwa mwanamke mwingine, Wema angeweza kufanya maamuzi ya kuleta masikitiko.

Tukumbuke, maisha siyo barabara iliyonyooka.
Patakuwa na mashimo; makorongo; na mitihani.
Kuchekana na kunyoosheana kidole kunaweza kuleta athari na hasara kubwa sana.

Tujadili

Together We Can Make it Happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *