Ukatili wa kijinsia kupitia mitandao ya kijamii
TOKEA ulimwengu ulipoingia kwenye karne ya kidijitali, pameanza aina kadha za jinai zikiwemo:
■ Ukatili wa udhalilishaji kupitia mitandao ya kijamii au Kimombo, wanaita Trolling
Hii hutumika kwa njia ya-
▪︎ kumtusi mtu au kundi la watu, kuptitia mitandao ya kijamii, mfano Twitter; Instagram; Facebook; Club House; nk.
▪︎ kutoa taarifa za uongo; zenye kuvunja staha; heshima; hadhi; utu; wa mlengwa/victim wao, kupitia mitandao ya kijamii.
▪︎ kutengeneza kanda ya video clip ya uongo juu ya mlengwa wao, mfano wanachukua kanda ya video clip ya watu wanaofanya tendo la ngono, afu wanabandika sura ya mlengwa wao kwenye mwili wa mmoja anaefanya maigizo kwenye kanda ya video clip ya ngono.
Hii kwa nia ya kumchafulia hadhi; heshima; staha; utu; wa mlengwa wake.
▪︎ kubandika sura ya mlengwa kwenye picha za mtu anaeonesha utupu wakati wa tendo la ngono, hasa ngono ya kinyume cha maumbile.
Hii wanafanyiwa wanawake zaidi, hata wanaume pia wanakuwa waathirika.
■ Kutumia mitandao ya kijamii, mfano Facebook, kwenye mburuzo au tagging, huku mjinai alietenda hivyo, anabandika video clip za ngono.
■ Kutumia jina bandia kwenye mitandao ya kijamii, na kumtusi; au kumkebehi; au ‘kumvua nguo’ mlengwa wake.
■ Kutumia rogue YouTube channels na kumfanyia kashfa mlengwa.
■ Kusambaza uongo juu ya mlengwa, ili kumchafulia hadhi; staha; heshima; utu; wa mlengwa, kwa nia ya kumchafulia fursa za ajira; au ndoa; au hata kuheshimika kwenye jamii.
■ Kutengeneza audio tape feki, na yeye hatumii sauti yake, anatumia sauti ya mwingine, na kumzushia mlengwa kila aina ya uovu na ubaya, ili atengwe na jamii; au akose ajira; au akose mtu wa kuwa naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.
Takriban mara nyingi, hubandika na picha ya mlengwa, eti ‘kutahadharisha jamii juu ya huyo mlengwa’.
Yeye, hataji jina lake; wala anwani; wala namba ya simu.
Utakuta hizo audio clip, na picha za mlengwa zinazungushwa kwenye mitandao ya kijamii.
Na wengi wanaosikiza audio clip feki, na kuona picha za mlengwa (ambazo mjinai kazitoa Facebook), huwa wanaamini uongo huo, na wao kuzisambaza.
■ Kubandika ‘tangazo’ feki kwenye watoaji huduma ya mitandao, mfano Google, na kuweka maneno ya kashfa na kudhalilisha kwenye hilo tangazo.
Mfano, anaweka jina la mlengwa, na kuwa anafanya biashara haramu ya ngono, yupo tayari kufanya aina yoyote ya ngono.
Mara nyingi mlengwa hana taarifa kuwa ameanikwa kwa njia hiyo kwenye mitandao, hadi apate Msamaria wa kumtonya.
■ Matusi ya nguoni kupitia Facebook; Twitter; Instagram; Snap Chat; Club House; na WhatsApp groups dhidi ya mlengwa/victim wake.
■ Kusambaza uongo juu ya mwanamke mwenye haiba; uzuri; ustaa; na sifa lukuki kuwa “Unamwona huyo? Ni lisagaji. Ndiyo maana tasa. Auliwe tu, asijekutuharibia binti zetu” .
Huyo, ni mwanamke anaeheshimika kwenye jamii anamoishi.
Anaheshimika kwenye jamii za dini.
Anaheshimika kwenye jamii za Asasi za Kiraia/AZAKI.
Anaheshimika kwenye mahekalu ya dini.
Anayo familia; marafiki; wafanyakazi wenzie; Tariqa/Usharika wa Ibada, yeye ni mmoja wa wakufunzi wa Mafundisho ya Dini.
Labda anapewa wari kuwasimamia kama somo.
Anapelekewa vijana na mabinti, kuwasimamia internship.
Mara nyingine, anaombwa kuwa Matron siyo tu wa Asasi za Kiraia/AZAKI; lakini kusimamia arusi.
Kwenye viliyo anasimamia Sala na Dua.
Basi huyo, anaweza kuchafuliwa, akasiginwa kwenye mavi na matope, hadi akijakuambiwa anashangaa “Huyo ni mimi eti?”
Uchafuzi huu unatumika kupitia mitandao ya kijamii.
■ Watoto wadogo wa kike na wakiume, kurubuniwa kupitia mitandao ya kijamii, na kunajisiwa.
Yapo makundi ya watu, zaidi wanaume, wanaonajisi watoto, wanaitwa paedophiles; na baadhi yao, hutumia mitandao ya kijamii.
■ Watu kutapeliwa fedha kwa njia ya mitandao ya kijamii, mfano, Kibubu Online.
Sheria
Taifa letu tulipitisha Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mitandao ya Kijamii 2015- Anti Cyber Crime Act 2015.
Sheria imewekwa iwe njia ya ulinzi kwetu; na pia njia ya kuwapa adhabu wajinai wa mitandao ya kijamii.
Bahati mbaya, taifa hatujawekeza vya kutosha, kutoa elimu jamii kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, juu ya hiyo Sheria.
Mwananchi akitendewa jinai hiyo, hajui aanzie wapi kushitaki, na kudai haki.
Bado, wananchi hatujaambiwa kuwa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, unaweza kufanyika; na unafanyika kupitia mitandao ya kijamii.
● Vitisho
● Ngono lazimishi
● Kuchafuliwa hadhi na staha na heshima
● Kufanyiwa utapeli wa fedha
● Watoto kughilibiwa kupitia mitandao ya kijamii
● Fitna na peke peke dhidi ya mlengwa, kwenye mitandao ya kijamii
Nini Kifanyike?
■ Wananchi wapewe elimu jamii juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii.
■ Sheria ya Makosa ya Jinai Kwenye Mitandao ya Kijamii/Cyber Crime Act 2015, iwekwe kwenye mitala ya mafunzo mashuleni.
Aidha, jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii, liwe somo shuleni.
■ Wanaovunja sheria kwa kutumia mitandao kwa ajili ya kutenda jinai, waadhibiwe stahiki.
Tukumbuke, mitandao ya kijamii pia inatumika-
▪︎ Kurubuni wasichana, na mara nyingine vijana wa kiume, na kuwauza kwenye biashara haramu ya uuzaji wa binadamu.
▪︎Kuibia watu pesa zao kwa ahadi hewa kuwa watawaingiza kwenye Freemasons ili watajirike.
▪︎ Kuibia watu pesa kwa njia ya biashara hewa- anaweka matangazo ya bidhaa kwenye mitandao ya kijamii, na picha nzuri kabisa.
Anakwambia upeleke pesa nusu, advance, afu humuoni tena.
▪︎ Wapo waliotapeliwa ‘uchumba’.
Mwanaume au mwanamke anatafuta mchumba.
Anapewa mapicha ya film actress wa mataifa ya nje.
Akija kumuona huyo mchumba, 😢.
Inawezekana kudhibiti ukatili wa kijinsia kupitia mitandao ya kijamii, iwapo sote tutatoa ushirikiano
Together We Can Make it Happen
Leave a Reply