MAWARIDI
MAWARIDI akiniletea kila baada ya kunipiga au kunitusi. Ni njia yake ya kuniomba radhi. Siku ya Wapendanao, Valentine’s Day, pia akiniletea mawaridi, na kuniambia nipake make up, ili kuficha alama za vidole vyake usoni mwangu. Pia akiniambia nivae nguo zenye kuficha alama za kipigo. Kila baada ya kunipiga, akilia na kuniomba “Baby nisamehe, sitorudia tena. Presha za maisha”. Siku zote, nilimsamehe. Jirani mwanaharakati aliona majeruhi akaniambia “Ondoka. Atakuumiza zaidi na zaidi”. Nikaangalia mawaridi juu ya meza, nikakumbuka “Baby I am sorry”, sikuondoka. Mawaridi kila wiki. Baadaye wiki mara 2. Mwisho, mawaridi kila siku na “Baby I am sorry. It won’t happen again”. Sasa ameniletea mawaridi 100. Kayaweka juu ya sanduku langu, wakati watu wanapita kuniaga. Nimepambwa, nimepakwa make up. Nguo nyeupe kama bi arusi. Ndugu zangu wanalia. Jirani mwanaharakati akasema “Ondoeni hayo mawaridi”. Wakamshangaa! Leo mawaridi sijui ndiyo ya mwisho? Bado analia “Baby, you are the love of my life”. Naondoka na mawaridi.
Together We Can Make it Happen
Leave a Reply