UKEKETAJI wa Mabinti/Wanawake
MWAKA 1998, Tanzania ilipitisha sheria kuharamisha masuala mengi ya jinai dhidi ya wanawake, moja wapo likiwa kuharamisha ukeketaji.
Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998 kwa mara ya kwanza, ilitambua:
▪︎ Uwepo wa ukeketaji
▪︎ Madhara yatokanayo na ukeketaji
▪︎ Ujinai unaotokana na ukeketaji
Tanzania ni miongoni mwa mataifa ya kwanza duniani, na ni Taifa la kwanza kuharamisha ukeketaji kwa kuweka Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998, na kurekebisha Kanuni za Makosa ya Jinai/Penal Code, pamoja na Vifungu vya adhabu kwa anayekutwa anashiriki kukeketa
Hata hivyo, jinai ya ukeketaji bado inaendelea hapa Tanzania, tena mara nyingine hufanywa na watu wenye upeo wa elimu.
Unasikia mwanaume akisema “mwanamke asiyetahiriwa ni lisagaji, hivyo, binti yangu lazima atahiriwe”.
Kauli aina hii inatoka kutoka kwa mwanaume mwenye elimu ya juu, na wadhifa serikalini na kwenye jamii.
Utakuta wanawake ambao siyo tu vijijini, bali hata kwenye majiji, wakifanya shopping na matayarisho ya binti zao kukeketwa.
Family huchangisha fedha kwa ajili ya ‘sherehe ya ukeketaji’.
Hapa JMT Bara, ukeketaji hutendeka kwenye mikoa takriban mingi, lakini zaidi kwenye mikoa ya:
▪︎ Arusha
▪︎ Singida
▪︎ Mara
▪︎ Kilimanjaro
▪︎ Dodoma
▪︎ Mwanza
Ukeketaji hufanyika kwa njia kadha:
1. Kukata kiua/clitoris. Hii hata baadhi ya jamii za Warabu hufanya, wanaita ‘suna’.
2. Kukata kiua na nyama za nje kwenye uke.
3. Kunyofoa vyote vilivyo nje ukeni, na kushona uke. Aina hii hubakisha kijitundu ili damu ya hedhi iweze kupita.
Binti anapoolewa, nyuzi hukatwa ili mume aweze kuingia.
Mume akisafiri, mwanamke hushonwa tena.
Huu mchakato wote ni kwa ajili ya:
▪︎ Kuzuia mwanamke asifaidi starehe ya tendo la ngono
▪︎ Kudhibiti mwanamke kimwili
▪︎ Kujenga fikra potofu kwenye jamii hizo kuwa mwanamke asiye keketwa anakuwa ‘mchafu’, najisi,
▪︎ Umejengeka utamaduni wa fikra finyu kuwa mwanamke ambaye hakukeketwa, atakuwa malaya
Orodha ni ndefu
MADHARA
▪︎ Afya ya uzazi SRH
▪︎ Maambukizi ya VVU
▪︎ Maumivu wakati wa ukeketaji na baadaye, mwanamke anapofanya tendo la ngono/ndoa, na anapijifungua mtoto
Bado ukeketaji unaendelea ulimwenguni na hapa kwetu.
Nini kifanyike kutokomeza ukeketaji?
Tujadili
Together We Can Make it Happen
Leave a Reply