Depression/Hisia ya huzuni
MARA nyingi, tunapopata changamoto au mitihani ya maisha, huwa inaambatana na hisia ya huzuni; unyonge; kupoteza furaha; na kujihisi ovyo ovyo.
Hisia hii ni aina ya hali ambayo inaitwa depression, na iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa na muathirika, na watu wa karibu yake, inaweza kujijenga kwenye akili; hisia; na mwili wa muathirika, hadi kuwa ni ugonjwa.
Depression inaweza ikawa ya muda, baada ya hapo, ikaondoka, pale muathirika anapopata msaada wa ushauri nasaha, sapoti, kutoka kwa wanandugu na rafiki.
Mara nyingine, depression huendelea kwa muda mrefu, hadi kugeuka ugonjwa.
Hapa ndipo muathirika anahitaji kwenda hospitali ili apatiwe msaada zaidi, hususan, msaada wa ushauri nasaha, pamoja na tiba ya dawa.
Depression huletwa na sababu kadha, zikiwemo:
▪︎ kupoteza ndugu au mke/mme kwa umauti
▪︎ kupitia ndoa kuvunjika
▪︎ kupitia misukosuko kwenye ajira
▪︎ mwanamke anapofanyiwa unyanyasaji wa kijinsia, ngono lazimishi, hadi kumfanya mwanamke kupoteza ari kwenye utu wake
▪︎ ajali ya gari au moto inayoleta athari au hata ulemavu, inaweza kusababisha depression
▪︎ hali ya ugonjwa endelevu, ambao tiba yake ni ngumu, inaweza kuleta depression
▪︎ Kudhalilishwa kwa sababu ya umasikini
▪︎ kukosa makazi
▪︎ kunyanyaswa ndani ya ndoa
▪︎ kufilisika mali
Sababu zipo nyingi, na takwimu zinaonesha kuwa kila mmoja wetu, atapitia hali ya kuwa na depression, japo mara moja kwenye maisha, hii haikwepeki.
Tunachoweza kufanya ni kutafuta msaada wa ushauri nasaha; tusijifungie peke yetu ndani; tujaribu kuangalia vipindi/sinema za kufurahisha; tuwe karibu na ndugu au rafiki mwenye uwezo wa kusaidia kwa ushauri.
Zaidi ya hapo, ibada na kumwegemea Mwenyenzi Mungu, ni muhimu mno.
Iwapo hali ya kuwa na depression inaendelea, ni vema kupata msaada wa kitaalamu kutoka kwa Washauri wa Ustawi Jamii au/daktari.
Usihisi aibu iwapo unapitia depression.
Usijihisi mnyonge.
Haupo peke yako.
Leave a Reply