Cyber Stalkers- Wakozi kwenye Mitandao ya Kijamii

Cyber Stalkers- Wakozi kwenye Mitandao ya Kijamii

PAMEANZA jinai mpya inayoambatana na ukuaji wa mitandao ya kijamii, inayotambulika kama Cyber Stalking kwa lugha ya Kingereza; au Ukozi wa Mitandao ya Kijamii.

Bado hapa JMT kwetu, hatujaweka sheria inayoainisha jinai hii, ya Ukozi wa Mitandao ya Kijamii, japokuwa jinai hii ipo, na inaweza kuhatarisha maisha ya wanajamii, hasa huyo mlengwa/target, wa ukozi.
Neno ukozi limetokana na maneno 2- Kozi Man au mpenda kupiga chabo ya kuangalia wenzake wanapokuwa kwenye utupu, wakioga bafuni; au wakiwa kwenye tendo la mapenzi au ngono, na kuchungulia.
Wangereza wanalo neno jengine, wanaita Voyeur au Mpiga Chabo.

Watu aina hii, voyeur, wanakuwa na sababu kuu 3 za kutenda uchafu huu:

■ Wanapata starehe kuchungulia wenzao wakiwa kwenye hali ya utupu wakiwa wanaoga bafuni, hasa mlengwa au target anapokuwa mwanamke na huyo voyeur ni mwanaume; na zaidi, pale ambapo alimtongoza huyo mwanamke, afu, akakataliwa.
Ndipo voyeur hutafuta kila njia ya ‘kumchungulia’ huyo mwanamke, kama njia ya kupata taarifa juu yake, na kuitumia taarifa hiyo kwa njia ya picha au kanda za video; au kuzusha uongo ili amchafulie jina na staha na hadhi kwenye jamii; au kama njia ya kumlazimisha/blackmail.

■ Mtu, mara nyingi anakuwa mwanaume, anapotongoza mwanamke, na kukataliwa, basi hutengeneza akaunti feki kwenye mitandao ya kijamii, na kumfanyia mlengwa wake kila aina ya istizai; na mara nyingine, kutunga kashfa za uongo, ili kumchafulia huyo mlengwa au victim wake.
Mara nyingine, mlengwa anakuwa binti mdogo, na hajui afanyeje, anaugua kimya kimya; au anaweza hata kufanya maamuzi hatari ya kujiua.
Kwa sababu bado JMT, hatujaweka mbinu na miundo ya kusaidia walengwa/victim wa ukozi wa mitandao ya kijamii.

■ Pale ambapo mtu yupo kwenye nafasi ya uongozi; au kwenye nafasi nyeti kama Usalama wa Taifa, na anapotumia nyenzo; miundo mbinu; vitisho; na dhima aliyokabidhiwa; kufanya maisha ya mlengwa/victim wake kuwa shubiri, hadi mlengwa kufikiria kuhama nchi; au kujiua.

Yote, hii ni kwa sababu hiyo Kozi Man/Voyeur anataka apate milki juu ya mlengwa/victim, kwa njia ya ukozi.
Watu aina hii, ya Ukozi, wanakuwa wapo tayari kumfanya mlengwa/victim wao apate ugonjwa wa akili; au ikibidi, apoteze maisha kabisa!
Wakozi ni jamii ya watu ambao starehe yao hupatikana kwenye kuwapa wenzao maumivu ya akili; hisia; hasa wanawake ambao waliwatongoza; au walitaka kuwadhibiti kingono, wakashindwa.
Nfipo hutumia-
▪︎ simu za viganja na namba za sim card feki, kuwapigia simu; afu kukaa kimyaaa.
Hii ni njia mojawapo ya tishio kwa mlengwa/victim

▪︎ kutengeneza akaunti feki kwenye mitandao ya kijamii, na kuomba urafiki kwenye Facebook; au kufanya follow kwenye Twitter; Instagram; nk.
Au kumtafuta kwenye WhatsApp group au JF au Google au Yahoo groups; afu ‘kumnyofoa’ to single out mlengwa/victim wake, na kumkandamiza kwa maneno/trolling; au kumkashifu: au kumtukana matusi ya nguoni.

▪︎ Kujiunga na magrupu ya mlengwa/victim wake huko Facebook, huku Mkozi akitumia akaunti feki, na kumburuta/tag huyo mlengwa/victim wake, pamoja na picha au kanda za ngono.

Hii yote, kumvunjia heshima na staha na utu wa mlengwa/victim wake.

■ Pale ambapo Mkozi hutunga uongo, kumchafulia mlengwa/victim wake, kumharibia ndoa; au mahusiano ya kimapenzi; au ajira; au biashara; au mahusiano yake na wanandugu na wanajamii.

Mkozi au Voyeur, takriban siku zote anataka kufahamu nani anamlala nani; au yupi kakorofishana na nani; cha kutisha zaidi, anataka kujua mapungufu ya wenzie ili aweze kuwa na msuli mkubwa zaidi, wa kuutumia, kwenye uhalifu anaofanya.
Bahati mbaya, JMT hatuja ainisha jinai hii kuwa ni jinai, na hatujaweka bayana aina ya jinai hizi zinazotumia mitandao; au simu; au barua pepe; au magrupu; jinai ambazo ni za kutisha; na ni za hatari sana.

Walengwa Wakuu wanakuwa wanawake, hasa anapotongozwa na Mkozi/Voyeur, afu akakataliwa.
Binafsi ishanitokea.

Hii makala waione

• Mhe Nape
• Mkuu wa TISS
• Mkuu wa TCRA
• IGP

Leila Sheikh
June 1, 2022

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *