Chujio la Socrates
MWANAFALSAFA wa Yunnani, Socrates, alikuwa ana kipimo ambacho alikipa jina chujio.
Kipimo hiki, kilikuwa kimewekewa pande 3, ambazo ndiyo mizani ya hilo chujio, ili wasikizaji waweze kupata taarifa yenye uhakika.
Pande ya Kwanza
Je, umeweza kuhakikisha kuwa unayoyasema juu ya mtu yanaukweli?
Na kama yanaukweli, ulitumia mbinu zipi kufafanua, na kujihakikishia kuwa ni ukweli?
▪︎Ulishuhudia kwa macho yako?
▪︎ Anaeongelewa kwenye hiyo tamthiliya au kisa, ndiye aliekupa taarifa hiyo?
▪︎ Umethibitishiwa na watu wasiopungua 7, kuwa wao, walishuhudia kwa macho yao, na juu ya hili, hawana budi bali kuamini.
Pande ya Pili
▪︎ Je, hata kama hiyo taarifa ni ya ukweli, itaongeza thamani ipi kwenye maisha ya binadamu; na kwa jamii kwa ujumla.
▪︎ Je, taarifa hiyo inaweza kuleta vurugu; ugomvi; mifarakano; iwapo itaanikwa mbele ya kadamnasi?
▪︎ Je, hiyo taarifa inaweza kuunganishwa na taarifa nyingine, hadi huo msalsal ukawa mrefu, na kupoteza maana kabisa.
Maana kila asikiae anapoongezea msalsal/chain, naye anaongeza chumvi; limao; bizari, hadi kupoteza ukweli uliokuwepo?
Hata kama ukweli ni punje ya hardali.
Pande ya Tatu
▪︎ Usipoongelea hilo suala kwa wanajamii, hadi kufikia kadamnasi, utapata hasara yoyote?
▪︎ Umepima matokeo ya kutoa taarifa hiyo, kwa mtajwa/mhusika wa hiyo taarifa?
Mara nyingine, unaweza sababisha mtajwa kupata majonzi na simazi, ambayo inaweza kuathiri afya yake huyo mtajwa. Anaweza hata akaamua kuaga dunia.
Ukishapima haya yote kwenye chujio na bado unahisi kuwa ni lazima uyaongelee masuala ambayo huna uhakika nayo, jaribu kujiweka kwenye nafasi ya mtajwa, na ufikirie majonzi na masikitiko utakayopata, ingekuwa wewe.
Iwapo bado unahisi ni lazima uyaseme, basi utambue kuwa hapa, pameingia suala la Stua Roho, yaani, unafanya kwa makusudi, ili umkomoe mtu.
Cha kusikitisha, hili chujio halitumiwi, siyo tu miongoni mwa wanajamii; bali hata serikalini na kwenye vyombo vya usalama.
Bila ya kujali athari, au kwa makusudi kwa sababu anafahamu athari na anataka kumchafulia mtu, basi utakuta inatungwa msalsal/chain wa alinacha, tena mara nyingine na watu wazima wa umri; na wenye vyeo vya kuheshimika kwenye jamii; lakini atatunga msalsal/chain wa uongo.
Chujio la Mwanafalsafa Socrates, linahitajika, la sivyo, wenye ‘sikio’ la Wakuu watatumia vibaya fursa hiyo.
Together, we can make it happen
Leave a Reply