Wanawake Kupeana Sapoti

Wanawake Kupeana Sapoti

UMOJA ni nguvu, ni usemi wa Kiswahili, na ilikua Kauli Mbiu ya Taifa letu baada ya Uhuru.
Umoja ni nguvu kama Kauli Mbiu iliweza kujenga Taifa madhubuti kabla na baada ya Uhuru wa Tanzania.
Aidha, maudhui hayo yamejenga jamii zetu wakati wa makarne ya nyuma, kwa kuweka mfumo wa kusaidiana miongoni mwa wanajamii, wakati wa msiba; kuumwa; kwenye ujenzi wa nyumba- wanajamii wa kitongoji walijumuika kusaidia kukandika kuta za nyumba; na wakati wa furaha, walijumuika kushereheka pamoja.

Wanaharakati wa haki jinsia tumeweka mfumo wa Umoja/Collective ambao ni njia au mfumo muhimu wa kujumuika ili kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii zetu, kwa kutetea uwiano wa jinsia.

Kwenye jamii zetu, palikuwepo na mfumo wa upato, ambao sasa wanaita vibubu au vikoba; mfumo wa tariqa na usharika wa Imani ambapo wanajumuia husaidiana; na vikundi au umoja wa kusaidia wasiojiweza, kama watoto yatima.

Ngoma kama lele mama pia zilikuwa ni mfumo wa tariqa kupitia sanaa.
Huu mfumo umeweza kujenga jamii madhubuti, na zenye msaada na huruma.

Wanaharakati tumekuwa na Umoja/Collectives ambazo zimejikita kwenye kutoa utumishi kwenye jamii.
Utumishi huu unajumuisha elimu jamii; msaada wa kisheria; ushauri nasaha; ukusanyaji wa vitu muhimu wakati wa majanga yasioepukika, na kuwapelekea wahanga; na kujenga familia zenye maadili.

Tatizo lilitokea pale ambapo baadhi ya wanajumuia/Collectives, walipogeuza nyanja hizo kuwa mali binafsi.
Hapa ndipo palitokea mpasuko!
Mpasuko huu umeathiri mfumo, umeleta mfarakano; umesitisha huduma zilizokua zikitolewa kwa walengwa; na umevunja mfumo mzima wa Umoja.
Hii ilitokana na ubinafsi miongoni mwa baadhi ya viongozi, hususan wa asasi za kiraia/AZAKI/civil society organisations; na hata kwenye tariqa na usharika wa kidini.
Tumeshindwa kutofautisha kati ya utumishi na maslahi binafsi.
Hii imeleta kutokua na afya au kufariki kwa asasi za kiraia/AZAKI/civil society organisations.

Kuporomoka huku kwa asasi zilizoundwa kwa ajili ya utumishi kumeathiri huduma kwa jamii.

Tukabaki kulaumiana; kuzushiana peke peke; kuchukiana; na kuua Dira na Azma ya asasi za kiraia.
Matokeo yake, walengwa wanakosa huduma muhimu ambazo ndiyo lengo haswa la uundaji wa asasi za kiraia/AZAKI/civil society organisations.

Nini Kifanyike?

● Waasisi wa asasi za kiraia/AZAKI/civil society organisations wakutane na kujadili wapi tumekosea

● Turudie Dira; Azma; Malengo; vilivyotupelekea kuanzisha vyombo hivyo

● Tujitathmini wapi tulikosea

● Tuangalie uwezekano wa kufufua hamasa zilizopelekea asasi hizo kuundwa

● Kukubali kutojiingiza kwenye masuala ya siasa, sisi, tunaweza kufanya utetezi kupitia Mikutano ya Majadiliano/Consultative Meetings na viongozi wa serikali; viongozi wa dini; nk

● Tuamue kuweka maelezo juu ya Mwanaharakati. Pametokea wimbi la wanaojiita wanaharakati, ambao sisi tunawaona ni wanasiasa; au wachochezi

● Turudie Kiapo tulichochukua miaka hiyo ya nyuma kuwa sisi hatutajiingiza kwenye masuala ya vyama vya siasa; hatutaleta vurugu; na tutafanya harakati ndani ya misingi ya sheria.

Iwapo sheria inayo mapungufu, tutahamasisha sheria irekebishwe.
Tulihamasisha sheria zirekebishwe miaka ya nyuma, na tukafanikisha.
Tena ndani ya Umoja na makundi yote ya jamii.

Ladies tujadili,

Together We Can Make it Happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *