Wanawake Wanapogeuzwa Bidhaa
TOKEA dakhari zamani, wanawake/wasichana, wamekuwa wakifanywa aina flani ya bidhaa.
Hii inajumuisha:
■ Kuozeshwa kwenye umri mdogo na wazazi, ili wazazi wapate mahari kama faida ya kumpa mwanaume mzee, binti wao mdogo kwa kisingizio cha mahari.
■ ‘Kuuza’ mabinti kwa dalali kutoka miji mikubwa na majiji, kufanya kazi za nyumbani, na mara nyingi, huuzwa kwenye biashara haramu ya ngono, bila wazazi kufahamu kuwa mabinti zao wanakwenda kufanyiwa ukatili wa uuzaji binadamu kwenye biashara haramu ya ngono.
Kwenye muktadha mwingine, wanawake wamekuwa bidhaa kwa njia zifuatazo:
● Kutumiwa kama chambo kwenye mabango; video; ya matangazo ya biashara ili kuvutia watazamaji.
Tangazo la gari au friji, linakuwa na picha/taswira ya mwanamke ambaye yupo nusu uchi.
Hii inaitwa click bait.
Gari lauzika kwa wateja wanaume pakiwepo na mwanamke mrembo, lakini aliye nusu uchi.
● Video vixen- pale ambapo mastaa wa Bongo Fleva wanapotumia wasichana, mara nyingine wamevaa kamba kamba tu, au shanga, kucheza kwenye kanda za video.
Muimbaji, takriban mara zote ni mwanaume, amekuwa amevaa nguo zake za staha.
Anayefanywa bidhaa ya kuuza kanda ya video ya nyimbo ni mwanamke/wanawake walio kwenye hali inayokaribia kuwa uchi kabisa.
● Ngoma wakati wa arusi; au wakati wa siku kuu; zinazochezwa, na kuwaweka wanawake kwenye hali ya utupu.
Hatuelewi kama hawa wanawake hupewa mihadarati wapoteze fahamu za utu hadi kuvua nguo hadharani, au hulipwa fedha nyingi, hadi kukubali kucheza hadharani kwenye hali ya kuwa uchi wa mnyama.
● Mabinti kughilibiwa wachukue selfie wakiwa uchi wa mnyama; mara nyingine kujikokomeka chupa kwenye sehemu za siri, na kuzipeleka kwa ‘wakala’ ili wapatiwe ajira kwenye music na film industry.
Kumbe wanadanganywa.
Hao ‘mawakala’ ni makuwadi wa kuuza kanda za video aina hiyo.
Kazi kwenye film na music industry inahitaji usajili BASATA, na kitambulisho.
Aidha, hao wanaowania fursa hizo, huitwa kufanya audition, ndiyo wapewe.
Orodha ni ndefu, ya wanawake/wasichana kugeuzwa bidhaa.
Tujadili,
Together We Can Make it Happen
Leave a Reply