Ugaidi wa Kidijitali

Ugaidi wa Kidijitali

JINAI ya ugaidi wa kidijitali, bado hatujaupa:

▪︎ Jina
▪︎ Utambulisho kuwa upo, na unaleta madhara makubwa kwa walengwa/victims
▪︎ Uainishi
▪︎ Fungu kwenye Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mitandao ya Kijamii
▪︎ mbinu za kutambua jinai hii inatokea na hatua za kuchukua iwapo tunalengwa sisi kwenye ugaidi wa kidijitali
▪︎ Kuwa wanawake watu wazima, na mabinti, ndiyo wanakuwa waathirika wakuu wa ugaidi wa kidijitali
▪︎ Kuwa jinai hiyo inaweza kutendwa na mwanaume; au na mwanamke; au na kundi la watu

Kwa nini jinai hii inashika kasi?

▪︎ Mitandao ya kijamii inaongezeka, na watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaongezeka

▪︎ Urahisi wa kupata simu ya mkononi, na kuweka applications/nyenzo za kutenda jinai hiyo

▪︎ Chuki binafsi zimepelekwa kwenye mitandao ya kijamii, ili kumkomoa au kuwakomoa walengwa

▪︎ Ule utamaduni wetu wa kunyoosheana vidole, tumeupeleka kwenye mitandao ya kijamii, na sasa, sehemu kubwa zaidi ya jamii tunaweza kuwafikia kwenye muda/dakika chache, kuliko ule umbea wa zamani, kabla ya uwepo wa mitandao ya kijamii

Mitandao ya Kijamii kutumiwa kama silaha ya kubomoa maisha ya mlengwa/walengwa

Hii inatokana na Kukosekana uratibu wa utumiaji wa mitandao ya kijamii.
Sheria ya Makosa ya Jinai ya Mitandao ya Kijamii, bado haijaainisha kuwa kutumia ugaidi wa kidijitali, siyo tu ni kosa la jinai, bali pia huleta athari kubwa kwa mlengwa/walengwa.
Mpaka imefika mahali, watu wanaishi kwa khofu kuwa wanaweza kuzushiwa uongo, ukamwagwa kwenye mitandao ya kijamii, na kuathiri:

▪︎ Hadhi
▪︎Staha
▪︎ Heshima
▪︎ Utu
▪︎ Ajira na ujira wetu
▪︎ Mahusiano ya kindoa au kimapenzi au na wanandugu na rafiki; na jamii kwa ujumla

▪︎ Kukuchafulia na kuzuia fursa za kupata ajira

▪︎ Kukomoa!

Wajinai wa ugaidi wa kidijitali wanazo tabia na hulka hizi:

▪︎ Wanakuwa na uovu wa kuharibu; kuvunja; badala ya kujenga

▪︎ Wanataka kuwa na mamlaka juu ya mtu/watu

▪︎ Wanapenda kuona walengwa/victim wao akiteseka

▪︎ Wanataka kuathiri afya; hisia; ajira; maisha; mafanikio; furaha; nk za mlengwa/victim wao

▪︎ Wanajiona wana uwezo wa kubomoa bomoa, na hiyo, ndiyo starehe yao

 

Wapo wengi tu ambao wamepata vitisho/blackmail kutoka kwa gaidi wa kidijitali, na wanaugua kimya kimya.
Hawajui wafanyeje.

Mimi, Leila Sheikh, ni mhanga/survivor wa gaidi wa kidijitali.
Nilitongozwa na mwanaume, nikamkataa.
Badala yake, nikachagua mwanaume mwingine, kumpa pendo langu.

Dah!

Huyo gaidi wa kidijitali alifanya kila aina ya jinai na njama na matendo, kwa kufikiri atanikomesha.

Nilifikiria nichukue wanaharakati 5 niende nao ofisini kwake tumpashe.
Nikawaza tutachukuliwa kama mashangingi wa rusha roho.
Badala yake, I called him out, mbele ya Wakuu wake wa Kazi, and told him to Eff Off.

Hakutegemea.
Alifikiri nitapata mental breakdown.
Au nitahama nchi.
Au nitajiua.

Nilichofanya, ni kumzungusha kama pia.
Alisahau mimi ni mwanahabari nguli, an expert in Investigative Journalism; Research; Mapping.
Award winning Investigative Journalist.
Award winning Author.
Award winning Film Maker.
Nikatumia mbinu na mtandao aliotumia yeye.
Kidogo apate yeye mental breakdown.

Saasa, JMT panahitajika kuwepo:

▪︎ Mafunzo kwa wanafunzi wa sekondari na vyuo, juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii

▪︎ Mafunzo kwa wanawake jinsi ya kukabiliana na gaidi wa kidijitali

▪︎ Marekebisho madogo kwenye Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Kijamii, ili kulinda wananchi, dhidi ya ugaidi wa kidijitali.

Mutajiuliza kwa nini nimeipa jina Ugaidi wa Kidijitali jinai hii?

Sababu ni hizi:

▪︎ Mbinu za kubambikiza khofu kwa walengwa/victims ni kama zile za ugaidi wa kisiasa

▪︎ Ile hisia ya kuwa na mamlaka juu ya mlengwa/victim ni kama ya ugaidi wa kisasa

▪︎ Kutokujali matokeo na hasara kwa mlengwa/victim

▪︎ Vitisho

▪︎ Ikibidi, kummaliza kabisa mlengwa/victim

Inawezekana kukabili jinai, dhulma hii, iwapo tunaamua kama Taifa.

Together, we can make it happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *