Kuambukiza VVU kwa Makusudi
MWAKA 2008, Tanzania tulipitisha Sheria ya Kudhibiti Maambukizi ya VVU.
Sheria hii tuliipitisha baada ya kupitisha Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI 2001.
Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI 2001 ni Sera ambayo ilileta:
■ Muongozo
■ Dira
■ Mbinu
juu ya kukabili VVU/UKIMWI.
Aidha, Sera hii imeainisha yafuatayo:
● Uwepo wa ugonjwa wa VVU/UKIMWI kwenye Taifa letu
● Jinsi ya kujikinga, dhidi ya maambukizi ya VVU/UKIMWI
● Mbinu za kutoa elimu jamii kwa wadau wote juu ya njia za maambukizi ya VVU; na aina za kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.
● Kuwapa nyenzo wahudumu kwenye sehemu za tiba, hata tiba asilia na jadi; juu ya VVU, na jinsi ya kukinga wagonjwa wasiambukizwe wakati wanapata tiba ya magonjwa mengine.
Mfano, Tabibu wa jadi wameelekezwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya VVU wakati wa kutoa chanjo za asili, watumie nyembe mpya kwa kila mgonjwa.
Kwa wahudumu wa hospital za kisasa, nao wameekewa Muongozo wakati wanatoa huduma.
● Kutokomeza unyanyapaa dhidi ya WAVIU- Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.
Kipengele hiki ni muhimu mno, na kimesaidia kuondoa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya WAVIU, kwenye maeneo yote ya maisha.
Hadi sasa, VVU unachukuliwa kuwa ni ugonjwa ambao yeyote anaweza akapata, iwapo hakuchukua tahadhari kadha.
NB:Na baada ya ujio wa ugonjwa wa COVID, ugonjwa wa VVU umeonekana ni rahisi kuchukua kinga; na kukinga wenzetu; tukilinganisha na ugonjwa wa COVID, ambao hatukutambua upo wapi, na saa ipi tunaweza kupata maambukizi.
Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI imeondoa kabisa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya WAVIU.
Wakawa hawafukuzwi kwenye ajira; pango la nyumba; hafla; mahekalu ya ibada; nk.
Serikali ilishirikiana na wanaharakati wa haki za binadamu kwenye mchakato huu, hadi sasa, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya WAVIU haupo tena.
Tabia ya kunyoosheana kidole ikapungua, hadi kutokomea kabisa.
● Sera imeweka misingi ya hadhi; staha; heshima; utu; wa WAVIU.
Aidha imeweka Vifungu muhimu juu ya Faragha na Stara kwa WAVIU.
Tanzania tumekua mstari wa mbele kwenye hili, na matunda tunayaona.
● Utoaji wa tiba ya ARVs ya kupunguza makali ya VVU/UKIMWI umewekewa Fungu kwenye Sera.
Mwaka 2010, tulikerekebisha Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI na kuongeza Vipengele kadha, vikiwemo Kuainisha Uwepo wa Makundi Maalum kwenye Jamii Zetu.
Hawa ni:
▪︎ Wanajidunga sindano za dawa za kulevya.
▪︎ Dada Poa, wanaofanya kazi ya ukahaba wa kuuza ngono.
Na wateja wao wanaonunua ngono.
▪︎ Dereva wa malori wa masafa marefu.
▪︎ Mashoga.
NB: Mimi niliongoza Timu za Afrika Mashariki za tafiti ili haya Makundi Maalum-Key Populations yawekewe Vifungu Vifungu kwenye Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI, ili wao wapate huduma ya ARVs.
Palitokea vuta nkuvute kuhusu haya Makundi Maalum, kuwa tunatetea vitendo hivyo; lakini kwenye jamii wapo, na inabidi tuwape huduma ya tiba kama wananchi wengine.
Hilo tu.
Mwaka 2008, tulipitisha Sheria ya Kuzuia na Kudhibiti Maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Sheria hii ni muendelezo wa Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI 2001/2010, lakini imejinaisha masuala kadha yanayohusu VVU/UKIMWI, yakiwemo:
▪︎ Kunyanyasa na kunyanyapaa wenye VVU/UKIMWI.
▪︎ Utoaji huduma ya tiba kwa WAVIU na wasio WAVIU kwenye muktadha wa maambukizi ya VVU.
▪︎ Haki ya kuoa au kuolewa kwa WAVIU, na iwapo Kadhi au Padre/Mchungaji au Pandit au Karani wa Bomani anakataa kuwafungisha ndoa WAVIU, anaweza kufunguliwa mashtaka ya jinai.
Vipengele ni muhimu kwenye hii sheria.
Na pakawekwa Fungu kwenye sheria juu ya Kuambukiza VVU kwa makusudi.
Hii imefanywa kuwa kosa la jinai na anayekutwa na hatia, anaweza kupewa adhabu chini ya Kanuni za Adhabu ya Makosa ya Jinai- Penal Code.
Kipengele hili imekuwa taabu kwa mahakama kuweza kutoa hukumu stahiki, kwa sababu inabidi mlalamishi aweze kuiaminisha mahakama kuwa alikuwa hana VVU kabla ya mahusiano ya kingono, na mtuhumiwa.
Inakuwa rahisi zaidi kwa mahakama, kuweza kutoa hukumu iwapo alieambukizwa VVU ni mtoto; alienajisiwa; na kuambukizwa VVU.
Ndipo tuangalie binti wa Kahama, alienajisiwa tokea miaka 11 na mwanaume mtu mzima, hadi umri wa miaka 14, na kugundulika ameambukizwa VVU
Kwenye kesi hii, mtuhumiwa alihukumiwa Kifungo cha miaka 30 kwa ubakaji; na miaka 5 kwa kumwambukiza binti VVU.
Mjinai alikaa gerezani, huku wanasheria wake walipeleka Rufaa, mahakama ya Rufaa.
Mjinai, akashinda, na kuachiwa huru, kwa njia ya kiujanja ujanja kwa kutumia lugha ya ushahidi, na vipengele kwenye sheria Sasa,
• Binti amenajisiwa, tukumbuke mtoto chini ya umri wa miaka 18, anakuwa hana ridhaa kwenye masuala ya kingono.
• Binti ameambukizwa VVU.
• Binti amedhulumiwa haki mahakamani, kwa mjinai kuachiwa huru, na anaweza kuendelea kuwafanyia mabinti wengine.
• Binti anahitaji aanze matumizi ya ARVs.
• Binti anahitaji nasaha.
• Binti anahitaji kuendelea na masomo, mfano VETA, ili apate stadi, aweze kufanya biashara au aajiriwe, aweze kujikimu maisha.
Ana umri wa miaka 14.
Alianzwa kunajisiwa alipokuwa na miaka 11.
Together, we can make it happen
Leave a Reply