Je, Harakati za Ukombozi wa Wanawake Umetengeneza Mashoga?

BAADHI yetu tumekuwa wanaharakati tokea bado tunasoma shule, high school. Tulivutiwa na ile Dira ya: ▪︎ Haki kwa wote ▪︎ Usawa kwenye fursa za elimu; ajira; biashara; uongozi nk ▪︎ Ukakamavu kwa mabinti na wanawake, tusionewe; tusifanyiwe ngono lazimishi; tusibaguliwe ▪︎ Tupewe stadi za maisha ili tuweze kukabiliana na changamoto Sisi, wanaharakati wa Afrika, hususan Afrika Mashariki, tulikaa kwa pamoja, na...

DigitALL: Ubunifu na teknolojia kuleta Haki Jinsia

Ndiyo Kauli Mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani, Machi 8, 2023. Kwenye karne hii ya kidijitali, wanawake tumepiga hatua, siyo tu kwenye ushiriki wetu kuleta maendeleo jamii; bali hata baadhi ya wanawake kushika usukani kwenye ubunifu uliotokana na maendeleo ya kidijitali. Hapo hapo, tukumbuke kuwa siyo wanawake wote kwenye Taifa letu adhimu, ambao wanapata fursa ya kutumia...

DONDOO

■ Kwa nini wanawake wa Afrika, hususan hapa kwetu, tulianza kudharau vipodozi na virembesha vya asili, na badala yake, tukajiingiza kwenye virembesha vilivyojaa kemikali? ■ Mabibi zetu wakitumia virembesha asili, bila ya kemikali, na hawakuwa na makunyo usoni. Wakipendeza mpaka uzeeni. Sisi, tunanunua cream zenye kemikali; za bei kubwa; ambazo baadhi yao zinaleta athari kwenye afya zetu. ■ Mfano...

Criminal Justice/Haki kwenye Jinai

TAIFA letu adhimu limeanza mchakato wa kukusanya maoni ya wadau muhimu, juu ya Haki kwenye Jinai, au Criminal Justice, kwa lugha ya Kingereza. Haki ambazo sisi wananchi tunatakiwa kuwanayo na kufaidi, ni: ▪︎ Kuweza kuchukua za kisheria dhidi ya mtu/watu, waliotutendea kosa/makosa ya jinai. ▪︎ Uwezo wa kupeleka malalamishi yetu dhidi ya makosa ya jinai tuliotendewa, kwenye chombo...

MAONI

■ Wananchi tupatiwe elimu jamii juu ya maana na utekelezaji wa Criminal Justice/Haki kwenye Jinai. Hii ifanyike kupitia vyombo vya habari, hususan redio, ambayo ni chombo cha habari shirikishi, na kinawafikia 89%-93% ya walengwa; hata waliopo kwenye vitongoji ambavyo vipo kidogo na umbali. ■ Pawepo na Daftari la waliokutwa na hatia ya jinai ya unajisi wa watoto;...

Choko Choko Mchokoe Pweza

WASWAHILI huwa tunapenda 'misemo', siyo tu wakati wa maongezi na wenzetu, bali hata kwenye: ▪︎ Kanga- huwa tunaweka usemi wa mafumbo; au wakutoa salaa; au wa kusherehekea sikukuu kama Eid; au kuomba radhi; kumshukuru Mwenyenzi Mungu; na zaidi ya yote, kurusha makombora ya majibu kwa mahasimu wetu, ambao wametutendea ubaya. Wengi hujiuliza, hasa watu wa sehemu za...

Matusi ya nguoni

WACHACHE miongoni mwa wanajamii wa JMT, wanaelewa kuwa Matusi ya Nguoni ni Kosa la Jinai Hii imeainishwa kwenye Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998, kwenye Utangulizi, pale ambapo Sheria ya Makosa ya Kujamiiana SOSPA 1998, imeweka bayana kuwa SOSPA 1998 ni Sheria inayorekebisha Sheria kadha, juu ya masuala ya jinai ya kingono, ili kulinda heshima; staha;...

Mipaka kwa Watoto

TUNAPOWEKEA watoto mipaka kwenye mienendo ya maisha yao, tunakuwa tunakiuka haki zao za maamuzi? Au ni njia mojawapo ya kuwapatia watoto Muongozo juu ya: • Maadili • Heshima • Kutojiingiza kwenye mambo ya kiutuzima, wakati bado ni watoto • Ulinzi • Mfumo wa maisha utakaowajenga Wanaharakati tumegawana pande 3, tupo: ▪︎ Tunaoamini watoto wanahitaji Muongozo na Mafundisho ya Kiroho/Spiritual Guidance, ili wapate makuzi...

Wanawake Wanapogeuzwa Bidhaa

TOKEA dakhari zamani, wanawake/wasichana, wamekuwa wakifanywa aina flani ya bidhaa. Hii inajumuisha: ■ Kuozeshwa kwenye umri mdogo na wazazi, ili wazazi wapate mahari kama faida ya kumpa mwanaume mzee, binti wao mdogo kwa kisingizio cha mahari. ■ 'Kuuza' mabinti kwa dalali kutoka miji mikubwa na majiji, kufanya kazi za nyumbani, na mara nyingi, huuzwa kwenye biashara haramu ya...