Ukatili wa Kijinsia kwa njia ya matusi
WENGI wetu hatujaweza kuchanganua na kuweka matusi dhidi ya mwenza/intimate partner, kuwa ni njia mojawapo ya ukatili wa kijinsia
■ Tumelelewa na kufundwa kuwa Kudhalilishwa kwa kitumia maneno ya kashfa; matusi; yanayoumiza hisia, ni jambo la kawaida.
Tumefundwa kustahmili, hata kama tunaumia hisia.
■ Jamii zetu zimempa mwanaume rukhsa kumtukana mwenza/intimate partner; kumbeza; kumkebehi; kumfanya ajihisi dhalili, bila ya kujali hisia za mlengwa/victim wake.
■ Ukatili wa matusi unaweza kusababisha, na mara nyingi husababisha –
>Maumivu ya hisia
> Mlengwa wa matusi kupoteza ari ya kujiamini.
Anabaki na woga wa kutojiamini.
> Hupelekea kuua ndoto za mlengwa, kwa kumkatisha tamaa.
■ Ukatili wa matusi huleta simazi kwa mlengwa; na mara nyingine, husababisha ugonjwa wa moyo
▪︎ Shinikizo la damu
▪︎ Huzuni
▪︎ Kukosa hamu ya kula
▪︎ Kukosa himaya ya kujitunza
▪︎ Kukosa ari ya kuishi
■ Matusi ya nguoni ni silaha ambayo hutumiwa na baina ya wanajamii, kuumiza heshima; hadhi; staha; utu; wa binadamu wenzao.
■ Matusi ya nguoni hujumuisha na:
• Kutungiwa uongo
• Kufanyiwa kashfa juu ya faragha zetu, ili tuonekane viumbe dhalili kwenye jamii tunamoushi
• Kutunga kashfa za uongo, na kuzisambaza kwenye jamii, ili kumkomoa mlengwa.
Bahati mbaya, ukatili huu wa matusi ya nguoni, mara nyingi, unahusisha wanawake dhidi ya wanawake wenzao.
KUKOMOA mtu, kwa lugha ya mjini.
Together We Can Make it Happen
Leave a Reply