Ugonjwa wa akili

Ugonjwa wa akili

Ni suala ambalo huwa hatulizungumzii kwenye jamii zetu.

Huwa tunahisi ni jambo la aibu iwapo sisi wenyewe, au mwanandugu anatatizo la ugonjwa wa akili.

Ugonjwa wa akili upo wa aina kadha:

1. Schizophrenia, ugonjwa huu ni pale mgonjwa husikia sauti kichwani mwake, na huwa anasema na hizo sauti, huku jamii ikimwona anasema peke yake.

2. Anxiety Disorder, ugonjwa wa wasi wasi mara nyingi hukumba watu waliopitia misukosuko ya maisha, na hujikuta wanao ugonjwa wa wasi wasi.
Mgonjwa mwenyewe hajitambui kuwa anaumwa.

3. Bipolar Disorder, mgonjwa anakuwa na furaha nyingi, mara anaingiwa majonzi.
Ni ugonjwa ambao waathirika wanahisi aibu kutafuta tiba, na msaada wa ushauri nasaha.

4. Clinical Depression, ni pale ambapo mgonjwa anakuwa na hisia za majonzi, pasipo na sababu.
Mgonjwa anakosa hamasa ya kuishi.

Ugonjwa wa akili, unahitaji vipimo vya hospital, na tiba kutoka kwa wataalam.

Tukumbuke, ugonjwa wa akili siyo aibu, ni ugonjwa kama ugonjwa aina nyingine.

Iwapo yupo ndugu, au rafiki, au sisi wenyewe, tunahisi tunapata changamoto za afya ya akili, tusisite kutafuta msaada.

Ladies,
Tujadili ugonjwa wa akili.

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *