Waleteni Watoto Kwangu
Yesu/Eissa
WATOTO wanazongwa kutoka kila upande, hapa JMT kwetu.
Watoto hawapo salama.
Matendo ya ukatili dhidi ya watoto yanazidi kuongozeka, orodha ni ndefu:
■ Unajisi wa watoto umeongezeka kwa 80%.
Kuanzia ubakaji wa mabinti; hadi ulawiti wa watoto wa kiume.
Kila kukicha, tunapata taarifa ya matukio mapya ya ulawiti wa watoto wa kiume, na wa kike.
Wanaofanya hivyo, ni watu wanaoaminiwa na wazazi mfano, mwanandugu: mwalimu wa shule au wa masomo ya dini; jirani; baba wa kambo; mara nyingine, hata baba mzazi.
Watoto wapo hatarini kwenye Taifa letu.
■ Watoto kupigwa na walimu, hadi kupoteza fahamu.
Mimi, sitaki watoto wapigwe!
Zipo adhabu aina nyingine za kuwapa watoto, ili kuwafundisha nidhamu.
Watoto kupigwa na walimu, huleta athari nyingi, zikiwemo:
> mtoto kutoroka shule kwa kukhofu atapigwa na mwalimu/walimu.
> mtoto kugeuka mkiwa, na kukosa hamasa ya kusoma.
> mtoto kupoteza ari ya maisha, hadi ukubwani, anakuwa jinga jinga.
> mtoto kuchukia shule, kwa sababu anailinganisha shule na sehemu ya adhabu ya shuruba.
Na kwa nini mtoto apigwe na ajnabi, eti mwalimu, ndiyo kunampa huyo mwalimu/hao walimu kiburi cha kupiga watoto wetu?
Wao nani kupiga watoto, tena, mpaka sehemu za kichwani, kitendo ambacho kinaweza kusababisha umauti kwa mtoto.
■ Watoto kutojaliwa kwa kupewa muda na wazazi.
Badala yake, huwapa zawadi za bei kubwa, ili ‘kuwahonga watoto’.
Wazazi wapo kazini; mitaani; watoto wanalelewa na wafanyakazi wa nyumbani.
■ Watoto kupewa smartphone, ambazo wengi wao hutumia kuangalia filamu za X za kiutuuzima.
■ Watoto kusikia wazazi wanatukana matusi ya nguoni, na wao wanajifunza.
■ Watoto kufatwa na wauza mihadarati kama cocaine au fentanyl nje ya geti la shule.
Hatufatilii.
Hatuna habari kuwa watoto wanaingizwa kwenye mihadarati, kwenye mazingira ya nyumbani, au karibu na shule.
■ Watoto kutumiwa kama omba omba.
Wapo watu ambao huchukua watoto kutoka vijijini kwao, kwa kuwalipa pesa mfano 300,000 TZS, afu kuwaleta kwenye majiji, na kuwafanyisha kazi ya omba omba.
■ Watoto kuuzwa kwenye biashara haramu ya uuzaji wa binadamu kwenye biashara haramu ya ngono.
Watoto hawa huchukuliwa kutoka vijijini.
■ Watoto kugeuzwa ‘shamba’ la kuvuna viungo kama-
> Figo
> Moyo
> Macho
Nk
Viungo hivi wanauziwa matajiri wa Ulaya Magharibi na Marekani, ambao watoto wao wanahitaji kupandikizwa viungo ili kuokoa maisha yao.
■ Watoto kufanyishwa kazi za shuruba kwenye mashamba makubwa.
■ Watoto ‘kuajiriwa’ kama wafanyakazi wa majumbani, na kufanyishwa kazi bila huruma.
■ Watoto kugeuzwa ‘punda’ wa kubeba mihadarati/dawa za kulevya, kusafirisha mataifa mengine.
■ watoto ‘kuuzwa’ kwenye ndoa za utotoni, ili wazazi wapate mahari.
■ Watoto wa kike kukeketwa, japokuwa tumeharamisha ukeketaji.
Tujadili
Together We Can Make it Happen
Leave a Reply