DONDOO
■ Kwa nini wanawake wa Afrika, hususan hapa kwetu, tulianza kudharau vipodozi na virembesha vya asili, na badala yake, tukajiingiza kwenye virembesha vilivyojaa kemikali?
■ Mabibi zetu wakitumia virembesha asili, bila ya kemikali, na hawakuwa na makunyo usoni.
Wakipendeza mpaka uzeeni.
Sisi, tunanunua cream zenye kemikali; za bei kubwa; ambazo baadhi yao zinaleta athari kwenye afya zetu.
■ Mfano wanawake Waswahili wakitumia virembesha kama liwa; sandali; msio; maua ya mawardi; bizari ya manjano; na ufuta.
Hivi vikipondwa kwenye jiwe maalum, na hutumiwa kama scrub na moisturizer.
■ Mafuta ya nazi yakitumiwa mwili mzima, mpaka kwenye nywele; makanyagio; uso; mikono; ili kulainisha ngozi.
Na sasa, wazungu wanatumia mafuta ya nazi kwenye virembesha, na sisi mabwege, tunanunua kutoka kwa wazungu, wakati mafuta ya nazi kwetu ndiyo asili.
■ Mafuta ya parachichi ni mazuri mno usoni.
Hulainisha ngozi kuwa nyororo.
Tunangoja yawekwe kwenye vikebe na wazungu, tununue.
■ Tui zito la nazi ni kirembesha kizuri mno, na pia hulinda ngozi dhidi ya miale ya jua, ambayo huweza kusababisha saratani.
■ Maziwa; asali; samli; mdaa; vyote hivi ni virembesha.
■ Yai na asali na bizari ya njano ni face mask nzuri mno.
Hivi, wapi tulikosea, hadi kudharau asili yetu?
Tujadili
Together, we can make it happen.
Leave a Reply