Criminal Justice/Haki kwenye Jinai

Criminal Justice/Haki kwenye Jinai

TAIFA letu adhimu limeanza mchakato wa kukusanya maoni ya wadau muhimu, juu ya Haki kwenye Jinai, au Criminal Justice, kwa lugha ya Kingereza.
Haki ambazo sisi wananchi tunatakiwa kuwanayo na kufaidi, ni:

▪︎ Kuweza kuchukua za kisheria dhidi ya mtu/watu, waliotutendea kosa/makosa ya jinai.

▪︎ Uwezo wa kupeleka malalamishi yetu dhidi ya makosa ya jinai tuliotendewa, kwenye chombo muhimu cha polisi; na polisi kupeleka malalamishi yetu mahakamani.

▪︎ Kupewa fursa ya kusikizwa tukiwa mbele ya mahakama, bila kunyanyaswa, wala kufanyiwa uonevu.

▪︎ Sisi wenye nchi yetu tupatiwe elimu jamii juu ya mchakato wa kupata Haki kwenye Jinai.
Wengi wetu hatutambui; wala hatuna stadi za kuanzisha mchakato wa kudai Haki kwenye Jinai.
Bado tunaogopa mifumo na vyombo tulivyowekewa, kutupatia haki.
Wengi wanafikiri hatutopata haki hata tukitoa malalamishi yetu kwenye vyombo husika.

▪︎ Bado yapo mapungufu kwenye ‘upokezi’ wa malalamishi mfano,
> ubakaji
> kipigo cha wanandoa
> kuchafua hadhi; jina; staha
tunaamini hata tukitoa taarifa polisi, hatutopata haki.

▪︎ Wapo baadhi yetu wanaoamini ni bora kutoa malalamishi yetu kwenye mitandao ya kijamii, au kupitia vyombo vya habari; kuliko kufata mlolongo wa mahakama.
Hii inatokana na ile hoja, ambayo takriban mara nyingi huwa ni kweli, kuwa Mwenye Uwezo wa Kifedha; Hadhi kwenye Jamii; ndiye atakayepata Haki.
Kuwa sisi, tatakabwera hatutopata haki hata tukifata mrengo wa Haki kwenye Jinai.
Na wala siyo uongo.
Waswahili tunao usemi Masikini hana Ushauri.
Na mara nyingi, wenye kukosa Haki kwenye Jinai, ni sisi wanawake!

▪︎ Wananchi wenye ulemavu wa viungo na ngozi wenye mahitaji maalum kwenye mfumo wa kudai Haki kwenye Jinai, wawekewe nyenzo ili kuwawezesha kupata hiyo haki.
Mwanamke ambaye anaulemavu wa kusikia na kuongea, anapibakwa, anahitaji mkalimani wa lugha ya ishara, ili aweze kutoa ripoti polisi; na aweze kutoa machungu yake mahakamani.
Hivyo, wananchi wenye mahitaji maalum wawekewe mifumo itakayowawezesha kudai, na kupata Haki kwenye Jinai.

▪︎ Wanawake wote, hata wasomi na wanaharakati, tumeonewa wakati tunatafuta haki kupitia mfumo wa sheria.

Itaendelea..

Ladies wanajukwaa wenzetu kadha, watatuwakilisha Sauti Zetu Wanawake, kwenye huu mchakato wa kupata Haki kwenye Jinai.

Tunawaomba mutoe-
> Maoni
> Duku duku
> Mapendekezo
> Mifano ya kwetu wanawake kukosa Haki kwenye Jinai, ili pafanyiwe marekebisho.

Together, we can make it happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *