Nini Kifanyike Kutokomeza Mmomonyoko wa Maadili?
Wazazi/Walezi
▪︎ Watenge muda kila wiki kuwapa nasaha njema watoto na miongozo ya maisha ndani ya misingi ya maadili.
▪︎ Wasiwape watoto smart phone.
Badala yake, wawapatie watoto simu za vitochi, kwa ajili ya mawasiliano.
▪︎ Wawapangie watoto muda wa kuangalia luninga; muda wa mazoezi ya shule/homework; muda wa kufanya usafi wa nguo zao na mazingira yao; muda wa kufanya mazoezi ya viungo na kucheza.
▪︎ Watoe mfano mzuri kwa watoto, kwa kuacha matusi; lugha chafu; ugomvi; kusengenya watu.
Badala yake, waoneshe mfano unaofata maadili na itikadi.
▪︎ Unywaji pombe kiholela kwa wazazi, wapunguze.
▪︎ watoto wapangiwe kazi za kujitolea/community work, kama kusafisha mitaro; kuweka mazingira safi; kupanda bustani ya maua.
Hii itawajengea watoto himaya ya kuzingatia dhima.
Viongozi wa Imani
▪︎ Wakemee tabia chafu kwenye jamii, ambazo kwa sasa, zinatapakaa kwa kasi.
▪︎ Watoe maudhui yenye kujenga jamii madhubuti, zenye kuzingatia maadili.
▪︎ Waoneshe mfano kwa waumini, kwa tabia na mwenendo wao viongozi wa Imani.
Kiongozi wa Imani anaetongoza waumini, anakiuka miiko na mafundisho ya Misahafu Takatifu.
▪︎ Watumie fursa za mikusanyiko ya ibada, kuhubiri yaliyo mema.
Waalimu
▪︎ Wafundishe kwa maadili na weledi.
Mwalimu anayetongoza mwanafunzi, siyo tu anakiuka maadili, lakini pia anatenda kosa la jinai.
▪︎ Watoe ripoti polisi iwapo wanahisi au wameshuhudia mtoto kunajisiwa.
▪︎ Washirikiane na wazazi, kwenye kujenga ari ya kusoma kwa watoto.
▪︎ Wasitumie watoto kama wafanyakazi wao, kuwasafishia nyumba zao au kuwafulia.
▪︎ Watumie lugha isiyio na matusi wakiongea na wanafunzi.
Vyombo vya Habari
▪︎ Vitoe elimu jamii juu ya maudhui ya malezi ya watoto.
▪︎ Vifatilie pale ambapo jinai inatendeka, mfano wanenguaji kuvua nguo hadharani, na kufanya vitendo ambavyo vinasababisha jamii kupotoka, hasa watoto.
▪︎ Vikemee wasanii/wanenguaji wanaocheza utupu hadharani.
Serikali
▪︎ Wizara ya Habari/TCRA iongeze Kifungu kwenye Sheria ya Makosa ya Mitandao ya Kijamii, kitakachosisitiza vipindi vya luninga na YouTube, viwe na alama ya PG/Parental Guidance- MKW/Muongozo Kutoka kwa Wazazi, ili kuzuia watoto wasiangalie vipindi na filamu za X, za watu wazima.
▪︎ YouTube channel zinazoonesha wanajamii kwenye utupu, wakifanya tendo la ngono hadharani, zifungiwe.
▪︎ Wizara ya Utamaduni na BASATA itoe Muongozo juu ya vipindi ambavyo ni sahih kuangaliwa na watoto.
▪︎ Nyimbo zinazoshadidia uvutaji bangi; utumiaji mihadarati; uvunjaji wa amani; zipigwe marufuku.
▪︎ Sera ya Utamaduni tuipitie upya.
Utamaduni ni muhimu kuulinda usipotee, lakini tunayo mipaka ya kimila.
Ngoma za ndani, zisichezwe nje kwa kisingizio cha mkole.
Together We Can Make it Happen
Comments (2)
ASANTE SANA KWA MADINI. Mimi nimeondoka nia hii:▪︎ ” watoto wapangiwe kazi za kujitolea/community work, kama kusafisha mitaro; kuweka mazingira safi; kupanda bustani ya maua.
Hii itawajengea watoto himaya ya kuzingatia dhima.”
Mimi ni muumini wa #SamakiMkunjeAngaliMbichi.
Shukrani.
Ahsante sana Mama yetu Mlezi Dr RKW Jumuiya ya Tuko Sawa tupo Pamoja bega Kwa bega kupasa Sauti kuhusu huu Ufunza.
Nami nichangie Kwa kuiomba BASATA na COSOTA kusimamia Maadili ya Utamaduni Wetu hasta upende Wa Miziki,Densi,Nyimbo n.k zinazolinda Mila na Desturi zetu walizoishi Mababu zetu tofauti na Sasa Usayansi umetuondoa katika Uasilia WETU na ndo chanzo Kikubwa Cha Mmomonyoko Wa MAADILI Tanzania na kuigine.
Kwa mfano wasanii kuimba na kudensi wakiwa nusu Uchi na aina za Densi sizizoheshimu Utu Wa Mtu na kulinda Harmony endelevu.
Na pia maneno yasio na Haina katika Nyimbo na Miziki mbalimbali,Ili kulinda Mila na Desturi zetu zilizoheshimu ASILI Takatifu na kwenenda katika Mwenendo Mwema.
Maana kizazi Cha Sasa hivi kinazidi kuangamia kimaadili.
Sheria ziwekwe Kali kiasi ili tupone tusiangalie Pesa huku kizazi kinaangamia.