Ukatili dhidi ya Watoto

Ukatili dhidi ya Watoto

PAMEZUKA wimbi la ukatili dhidi ya watoto JMT Bara, na Visiwani.
Matukio yanatolewa ripoti kila kukicha, kuanzia:

▪︎ Unajisi wa watoto kingono
▪︎ Vipigo
▪︎ Vitisho
▪︎ Ngono lazimishi kwa mabinti wadogo
▪︎ Ulawiti wa watoto wa kiume
▪︎ Mateso ya kihisia kwa matusi
▪︎ Mateso kutoka kwa wazazi ambao huwapiga watoto bila kiasi, au huwaacha bila ya matunzo na usimamizi
▪︎ Kunyimwa haki ya kuendelea kusoma
▪︎ Ajira ya watoto

Orodha ni ndefu.

Tanzania tumeweka Sheria; Sera; Miongozo; juu ya Ulinzi wa Watoto, lakini licha ya uwepo wa nyenzo muhimu kama hizi tajwa, bado baadhi ya watoto wanakosa ulinzi.

Kama Taifa, tumefika mahala ambapo ni aibu kwenye jamii zetu, hata paka hulinda na kutunza wanae, seuze sisi, binadamu, tunawapa watoto mateso.

Hata kwenye malezi na makuzi, vijibinti vinafundishwa kucheza ngoma za vigodoro, badala ya kuwafunda wasome, wawe wakakamavu, wakue kwenye misingi ya maadili.

Binafsi, nilishawahi kumwambia dereva asimamishe gari, nikatoka, nikaenda kumnyanyambua mwanamke ambaye alikuwa amekaa na shosti zake kibarazani, wakati mtoto wake wa miaka 2 yupo katikati ya barabara, huku boda boda zinamwepa.
Mama hana habari, keshakunywa uji wa kungu, anatafuna gomba, mdomo unaenda kama santuri mbovu.

Nini kifanyike?

Tujadili

Together We Can Make it Happen

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *