Urembo Unapogeuka Athari Kwenye Afya
Tangu dahal zamani, wanawake wamekuwa wakitumia urembo wa vipodozi kama udongo mwekundu (ochre), samli, tui la nazi, nta au gundi la miti kwenye nywele, mdaa, na Vinginevyo ili wajipendezeshe.
Inasemekana kuwa Malkia Cleopatra akioga kwa maziwa ya punda ili kulainisha ngozi. Aidha, akipaka usoni samli iliyochanganywa na maua ili kuondoa makunyo ya uso.
Urembo ni sehemu muhimu ya wanawake.
Karne kwa Karne, wanawake wamekuwa wakijipamba na kila siku zinavyopita, wataalam wanagundua vipodozi vipya ili kuridhisha wateja wanawake waweze kujipamba.
Wajapani walikuwa wakijipaka unga wa mchele usoni na kuyapaka rangi nyekundu meno yao ili wapendeze.
Hadi sasa, vipodozi vimekuwa biashara kubwa ya fedha za mabilioni ya dola za kimarekani.
Vipodozi sasa vimeongezwa kujumuisha makalio bandia, matiti bandia, na kujibadili rangi ya ngozi.
Kwa kiasi kikubwa, maendeleo haya yameleta athari ya kiafya kwa wanaotumia vipodozi aina flani. Mfano Michael Jackson alijibadili hadi ilibidi uambiwe kuwa ndiye yeye.
Je, urembo lazima ulete athari? Au tunaweza kujiremba bila kuathiri afya zetu?
Je, nini hasa kinapelekea wanawake kutumia vipodozi ambavyo vinaweza kuharibu figo za mtumiaji vipodozi?
Tujadili
Together, we can make it happen
Leave a Reply