Gaslighting-Mafumbo Yakuumiza Hisia
TUMEJENGA utamaduni wa kurushiana mafumbo yanayoumiza hisia za wenzetu.
Kwa Kingereza, tabia hii inaitwa Gaslighting ambayo duniani kote, imejijenga kwenye tamaduni za binadamu, wanawake na wanaume.
Hapa kwetu JMT, gaslighting tumeipita majina kadha yakiwemo:
▪︎ Rusha Roho
▪︎ Mipasho
▪︎ Kuchamba
▪︎ Kusuta
▪︎ Kuchafua staha na heshima ya mwanajamii mwenzetu, kwa kuzungusha taarifa za uongo juu yake
▪︎ Masimango
Hii yote, ina nia ya kuumiza hisia za mlengwa.
Anaefanya gaslighting, anapata sukuun/raha, baada ya kuumiza hisia za mwenzake.
Kwa nini baadhi ya wanajamii hufanyia wenzao gaslighting?
▪︎ Kumfanya mlengwa wa gaslighting akose furaha na amani
▪︎ Kumnyanyasa na kudhalilisha utu wa mlengwa
▪︎ Kumsigina mlengwa na kumfanya ajihisi dhalili
▪︎ Kumvunja moyo na himaya na ari mlengwa
▪︎ Kumchafulia mlengwa staha na heshima yake kwenye jamii iliyomzunguka
▪︎ Kumkomoa mlengwa iwapo anamafanikio ya maisha
▪︎ Kwa wanaume, wanafanya gaslighting kwa wanawake waliowakataa baada ya kuwatongoza
Orodha ni ndefu, na yote haya kwa nia ya kuwapa gaslighters melki juu ya walengwa/victim wao; kuwadhalilisha; ili wao gaslighters wajihisi washindi.
Gaslighting inaendana na saikolojia ya baadhi ya watu kutaka kuumiza hisia za wenzao.
Hapo, ndipo wanapopata starehe yao.
Gaslighting hufanyika hadi miongoni mwa watoto.
Unaweza kuona mwanao amejikunyata; au anakataa kwenda shule; hufahamu sababu.
Na mara nyingi hatuliizi watoto kwa kituo, ili watwambie kuwa kipo kikundi cha watoto shuleni kwake kilichopania kumkosesha furaha.
Watoto wanaofanyia wenzao gaslighting, wamejifunza kwa watu wazima.
Mduru wa kuumiza hisia unaanza utotoni, na sisi bado hatujatambua kuwa huo mduru ni kinyume cha tabia nzuri, na mduru unaweza kupelekea mlengwa kuchukua hatua ya kujiua.
Huwa hatuzungumzii tabia ya gaslighting, na takriban mara zote, tunamcheka mlengwa wa rusha roho au mipasho au masimango.
Tunamchukulia mtenda gaslighting kuwa ni hodari; shujaa; mshindi.
Kumbe huyo mtenda gaslighting ni
▪︎ Hayawani
▪︎ Mkosa huruma
▪︎ Msungo wa tabia nzuri, za kujenga amani na furaha na mshikamano kwenye jamii. Ni kiumbe aliekosa adabu na unyenyekevu.
Gaslighting inaweza kuathiri hisia na fikra za mlengwa, na kumfanya akose hamasa ya kufaidi na kufurahia maisha.
Zinatungwa nyimbo za rusha roho ili kukomoana.
Binafsi ishanitokea.
Kwa vile mie ni MwaTanga, nilimrudishia makombora huyo mwanfulani, akaondoka saluni analia.
Baadaye, nilijuta.
Kama mwanaharakati, nilitakiwa nimpe salaa juu ya uovu na uharibufu wa gaslighting.
Siku hizi akiniona, ajificha kwenye mihogo.
Dah!
Tujadili
Together We Can Make it Happen
Leave a Reply